KUFUATI barabara kuu ya Morogoro-lringa kukatisha ndani ya hifadhi ya mbuga za wanyama ya Mikumi,wimbi la wanyama mbali mbali kugongwa na magari linazidi kushika kasi,ambapo juzi katimba mtandao huu ulishuhudia mnyama Nyati aliyegongwa na Fusso.
Hivi karibuni mwandishi wa Mtandao huu akiwa na usafiri wa pikipiki akitokea wilaya ya Kilombero alikatiza kwenye mbuga hiyo na kushuhudia wafanyakazi wa mbuga hiyo'Magemu' wakigawana minofu ya nyama ya nyati aliyegongwa na gari alipokuwa akijaribu kuvuka kuelekea upande wa pili wa barabara hiyo.
No comments:
Post a Comment