KATIKA
hali isiyokuwa ya kawaida, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA) Dk. Willibrod Slaa ametakiwa kutokanyaga mkoani
Mbeya kuanzia sasa hadi ifikapo mwaka 2015 wakati wa uchaguzi mkuu.
Kauli
hiyo imetolewa juzi mjini hapa na kundi kubwa la wanachama na wapenzi wa
CHADEMA mara baada ya kumalizika kwa mkutano mkubwa ambao umevunja
rekodi ya mikutano iliyowahi kufanyika kwenye viwanja vya Luanda-Nzovwe,
maarufu Uwanja wa Dk. Slaa.
Wamedai
kwamba hakuna haja kwa Slaa kwenda mkoani humo kwa ajili ya mikutano ya
kuhamasisha, badala yake wamemtaka atulie na kuanza maandalizi kabambe
ya timu ya uchaguzi mkuu ujao.
Bila
kutaja majina yao, wengi wa wanachama hao wamesema kumruhusu Dk. Slaa
kuzunguka mikoani katika operesheni ya M4C ni kumchosha bure kwa kile
walichodai anahitaji kukusanya nguvu katika mapambano makubwa ya safari
ya kuelekea kushika hatamu za nchi 2015.
“Tunamtaka Dk. Slaa mwaka 2015. CCM wanasema eti kazeeka, sisi vijana tunamtaka Dk. Slaa na uzee wake.
“Nchi hii
lazima iendeshwe na wazee wenye akili, hekima na busara, wazee wenye
kujua uchungu wa watu wanyonge kama mzee wetu awaonyeshe CCM jinsi nchi
ya wapigania haki inavyopaswa kuongozwa,” walisema vijana hao
waliojitambulisha kwa majina ya Saleh Issa, John Paul na mmoja
aliyejitaja kwa jina la Mussa.
Katika
mkutano huo ambao ulihutubiwa na Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho,
Freeman Mbowe, ulishuhudia baadhi ya wanachama wa CCM wakichangia
harambee ya papo kwa papo ambapo kiasi cha sh milioni 3.2 zilipatikana.
Baadhi ya
askari polisi walioshiriki kulinda mkutano huo, wamekiri kuwa
ulitawaliwa na utulivu wa hali ya juu tofauti na ilivyokuwa ikihisiwa na
walinzi hao wa amani.
Mkutano
huo wa juzi ulimalizika kwa chama hicho kusimika uongozi imara wa Kanda
ya Nyanda za Juu Kusini chini ya mratibu wake, Frank James Mwaisumbe,
mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Tumaini Iringa, aliyekuwa kada wa CCM ambaye
amejiunga na CHADEMA, Mwaisumbe aliangushwa katika kura za maoni mwaka
2010 alipogombea ubunge jimbo la Mbeya mjini kwa tiketi ya CCM.
Licha ya
kuwepo kwa mafanikio makubwa katika mkutano huo, baadhi ya wapenzi na
wanachama wa chama hicho walielezea kukerwa na nguvu za ziada
zinazoonyeshwa na vijana wa ulinzi wa chama hicho, Red Brigedi, na
kushauri wapewe mafunzo ya amani na uvumilivu ili kukisimamia vyema
chama hicho.
Tanzaniadaima
No comments:
Post a Comment