WAKATI
kondomu feki zilizopigwa marufuku Uingereza mwaka jana zikiwa katika
mzunguko nchini Tanzania, kesi za gonjwa la ngono hatari lisilotibika
zimeongezeka kwa asilimia 25 Uingereza, huku wataalamu wakionya kwamba
ugonjwa huo umekuwa sugu zaidi katika tiba.
Zaidi ya kesi 21, 000 za maambukizi mapya zimedaiwa kutambulika kwa mwaka 2011/12.
Kondomu hizo feki aina ya Trojan na Durex
zenye vipele vipele ambazo mwishoni mwa mwaka jana serikali ya
Uingereza iliingia katika msako mkali kusaka mamilioni ya kondomu hizo
bandia zilizokuwa zikiuzwa nchini humo miezi 18 iliyopita.
Kirusi kinachoambukiza ugonjwa huo hatari
kimetajwa kuwa ni 'Neisseria' ambacho ni tofauti na vingine ambavyo
mara nyingi hutibiwa kwa dozi moja tu ya viuavijasumu (antibiotics)
ambayo angalau hufanya kazi kwa asilimia 95 kiufanisi.
No comments:
Post a Comment