Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, March 24, 2013

HUYU NDO BINTI ALIYENUSURIKA KULA KICHAPO WAKATI AKIGAWA MSAADA KWA OMBA OMBA




MLIMBWENDE wa East Africa 2010, Anneth Kaguo, Jumatano iliyopita alinusurika kuchezea kichapo kutoka kwa vijana na watoto wanaoishi katika mazingira magumu ‘ombaomba’ katika maeneo ya Mnazi Mmoja jijini Dar.

Tukio hilo lilitokea saa moja usiku na kushuhudiwa na mwandishi wetu baada ya mlimbwende huyo kujikusanya na kwenda  maeneo hayo kwa lengo la kutoa msaada kwa vijana na watoto hao wanaojitafutia riziki zao mitaani.

Tofauti na matarajio yake, baada ya mrembo huyo kufika eneo hilo aliwakuta vijana na watoto hao wakiwa wachache, hata hivyo aliamua kuwapa nasaha za maisha kabla ya kuwapa alichowapelekea.

Ghafla, kundi lingine la vijana hao liliibuka na kujichanganya na wenzao hasa baada ya kusikia kwamba kulikuwa na msaada utakaotolewa.

No comments:

Post a Comment