Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, March 24, 2013

WAENDESHA BODABODA WAMUUA POLISI



Waendesha pikipiki maarufu ‘bodaboda’ wa Kijiji cha Ngwinde Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma wamemuua Polisi, Konstebo Yohana baada ya kumpiga na gongo kichwani, muda mfupi baada ya polisi huyo kumuua mwenzao, Makisio Nganyuni (25) kwa kumpiga risasi kwenye paji la uso. 
Tukio hilo lilitokea jana saa 5 asubuhi katika
barabara kuu iendayo Tunduru, Masasi baada ya waendesha pikipiki hao zaidi ya sita kumvamia askari pamoja na mwenzake, Venance Kamugisha waliokuwa katika pikipiki ya polisi.

Akithibitisha tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoani Ruvuma, Deus Nsimeki alisema polisi hao walikuwa katika mizunguko ya kawaida, walipofika katika Kijiji cha Ngwinde walikutana na Katibu wa CCM wa kijiji hicho, Shaban Ngae ambapo walianza kuzungumza naye.

“Wakati wakizungumza lilitokea kundi la waendesha pikipiki (bodaboda) zaidi ya sita wakiwa wamepakizana, walipowakaribia walianza kurushiana maneno na polisi,” alisema na kuongeza;

No comments:

Post a Comment