Frank Hillary, 27, aliyetambuliwa
kuwa mlokole, amethubutu na kuweza kukatisha maisha ya mama yake,
Ndolukasi Lugamo, 50, akitumia shoka kuondoa uhai wa mzazi wake.
KWELI
kuelekea mwisho wa dunia, mengi yataonekana. Mtu unawezaje kumpiga
shoka mama yako mzazi, aliyekutunza tumboni mwake kwa miezi tisa,
akakunyonyesha, kukusomesha hadi kukua na kujitegemea?
Tukio
zima, lilichukua nafasi Alhamisi iliyopita, Mtaa wa Malipula, Kata ya
Chamwino, mkoani Morogoro na inadaiwa kwamba kabla ya mauaji, Hillary
alimpiga vibao, mitama na mateke mama yake.
Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, Pili Athuman, alidai kwamba siku ya tukio, kulitokea mabishano kati ya Hillary na mama yake.
“Yalikuwa mabishano kidogo lakini ghafla yule kijana alimvamia mama yake na kuanza kumpiga,” alisema Pili na kuongeza:
“Yule kijana ni mtoto wa
pekee wa yule mama. Tunashindwa kuelewa mpaka sasa chanzo cha tukio
hilo. Halafu wale watu ni walokole kabisa na siku zote walikuwa wanaishi
kwa upendo.”
No comments:
Post a Comment