Papa
Francis akisalimiana na Rais wa Argentina, Cristina Fernandez de
Kirchner alipowasili Vatican, jana kuhudhuria sherehe za kutawazwa kwa
mkuu huyo wa Kanisa Katoliki zitakazofanyika leo. Picha na AFP.
Vatican
City. Ulinzi mkali umeandaliwa kwa viongozi mbalimbali wa kiserikali na
wale wa kidini duniani waliowasili jijini Vatican, kwa misa maalumu ya
kutawazwa kwa Papa Francis leo.
Waumini na wageni milioni moja
akiwamo Balozi wa Tanzania nchini Italia, Dk James Msekela, wanatarajiwa
kuhudhuria misa hiyo itakayofanyika kwenye Viwanja vya Kanisa Kuu la
Mtakatifu Petro.
Baada ya Papa Francis kutawazwa,
ataanza rasmi kazi ngumu ya kuliongoza Kanisa Katoliki lenye waumini
wengi na ambalo limekumbwa na mizozo kadhaa ikiwamo ya utovu wa nidhamu
kwa baadhi ya makasisi.
Kiongozi huyo alichaguliwa Jumatano
iliyopita kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Papa Benedict XVI,
aliyejiuzulu Februari 28, mwaka huu.
No comments:
Post a Comment