Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Saturday, March 23, 2013

JAMBO LEO BINGWA MPYA FAINALI ZA NSSF 2013



Naibu Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Amosi Makala, akimkabidhi kombe la Ubingwa wa michuano ya NSSF Media Cup naodha wa timu ya Jambo Leo, Said Mwishehe, baada ya timu hiyo kuifunga Changamoto bao 1-0 katika mchezo wa fainali uliochezwa leo asubuhi kwenye Uwanja wa TCC Chang’ombe jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Amosi Makala, akimkabidhi kombe la Ubingwa wa michuano ya NSSF Media Cup naodha wa timu ya Business Times 'Business Queens', Lulu Habibu, baada ya timu hiyo kuifunga TBC jumla ya mabao 39-18 katika mchezo wa fainali uliochezwa leo asubuhi  kwenye Uwanja wa TCC Chang’ombe jijini Dar es Salaam. 

 Mshambuliaji wa Jambo Leo, Julius Kihampa, akichuana kuwania mpira na beki wa Changamoto, Emmanuel Balele, wakati wa mchezo huo wa Fainali uliochezwa leo asubuhi kwenye Uwanja wa Tcc Chang'ombe. Katika mchezo huo Jambo Leo imeibuka na ushindi wa bao 1-0 na kutangazwa kutwaa kombe hilo la NSSF CUP 2013 na kuwa bingwa mpya wa michuano hiyo iliyomalizika leo.

No comments:

Post a Comment