Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe
(Mb.) akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu ziara
ya kitaifa ya siku mbili ya Rais mpya wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe.
Xi Jinping atakayoifanya hapa nchini kuanzia tarehe 24 hadi 25 Machi,
2013. Wengine katika picha ni Mhe. Mahadhi Juma Maalim (Mb.) (kulia),
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Bw. John Haule, Katibu Mkuu wa Wizara
wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Mhe.
Membe, Mhe. Maalim, Bw. Haule na Balozi Gamaha wakisikiliza swali
kutoka kwa Mwandishi wa Habari (hayupo pichani) wakati wa mkutano kuhusu
ziara ya Rais wa China, Mhe. Xi Jinping hapa nchini.
Mmoja
wa waandishi wa habari kutoka China akiuliza swali kwa Mhe. Membe
(hayupo pichani) wakati wa mkutano kuhusu ziara ya Rais wa China hapa
nchini
Waandishi kutoka mashirika mbalimbali ya habari ya China pia walikuwepo kwenye mkutano huo.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Balozi Rajab Gamaha (kulia) akiwa na Balozi wa Tanzania nchini China,
Mhe. Philip Marmo (katikati) pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora
katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Bertha
Semu-Somi wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani) alipozungumza na
waandishi wa habari kuhusu ziara ya Rais wa China hapa nchini
No comments:
Post a Comment