Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Saturday, March 2, 2013

Mzee Makamba anena:Mungu ataiadhibu CCM



Katibu Mkuu mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuph Makamba, 
 
Katibu Mkuu mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuph Makamba, amejitokeza na kubaini athari za kukithiri kwa ufisadi na rushwa ndani ya chama hicho. Makamba alishika wadhifa huo katika kipindi cha kuanzia Juni 2006 hadi Aprili 10, 2011, ambapo yeye na waliokuwa wajumbe wa Kamati Kuu (CCM) walijiuzulu.

Mbali na Makamba, wajumbe wengine walikuwa manaibu makatibu wakuu, George Mkuchika (Bara) na Saleh Ramadhan Feruzi (Zanzibar), Katibu wa Itikadi na Uenezi, John Chiligati.Wengine ni Katibu wa Uchumi na Fedha, Amos Makala, Katibu wa Mipango, Kidawa Saleh na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mambo ya Nje, Bernard Membe.

Hata hivyo, Makamba alikuwa miongoni mwa viongozi waliotajwa kukisababishia chama hicho kupoteza mvuto wake, miongoni mwa sababu zikitajwa kuwa kukithiri kwa tuhuma za rushwa na ufisadi.Lakini katika hafla ya kuitangaza halmashauri mpya ya wilaya ya Bumbuli wiki hii, Makamba, alieleza kukerwa na rushwa na ufisadi ndani ya CCM na serikalini. 

No comments:

Post a Comment