HATIMAYE ujenzi wa kiwanda cha kusafisha gesi kabla ya kusafirishwa kwenda Dar es Salaam umeanza mkoani Mtwara.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi alisema jana kuwa
ujenzi huo unaofanywa na Kampuni ya China Petroleum and Technology
Development Co-operation (CPTDC), ambao awali, ulipaswa kuanza wiki
iliyopita, umeanza juzi baada ya Serikali kufikia mwafaka na wananchi wa
Kijiji cha Msimbati kinapojengwa.
“Mkuu wa
Wilaya ya Mtwara (Wilman Ndile) na vijana wake walilazimika kufika
Kijiji cha Msimbati, ambako wananchi walikuwa na mgogoro na watu wa
Marine Park,” alisema Maswi.
Alisema
baada ya ziara hiyo kushindwa kufanyika Jumapili iliyopita, uongozi wa
wilaya ulikutana na viongozi wa kijiji na kufikia mwafaka uliofanikisha
kuanza kwa ujenzi huo.
Alisema
kuanzia mradi huo kutatoa ajira za kawaida kwa wakazi saba wa maeneo
yanayozunguka mradi huo na kwamba kazi hiyo itaongeza mahitaji ya bidhaa
mbalimbali na huduma katika Kata ya Msimbati
“Mathalan
kuku, matunda na mboga za majani vinahitajika sana. Sasa wananchi ambao
awali, hawakutaka kuelezwa lolote, wameanza kuchangamkia fursa hizo
jambo ambalo litawanufaisha zaidi,” alisema.
Ujenzi huo ulielezwa kuwa unatekelezwa sambamba na mwekezaji kujenga visima vitatu vya maji safi na salama kijijini Madimba.
Alisema
mwekezaji pia atasambaza umeme kwa kaya 300 za ndani na jirani ya kijiji
hicho na kwamba vifaa vitakavyotumika katika kazi hiyo vinatarajiwa
kuwasili mwishoni mwa mwezi huu.
Maswi
alisema shule zote kwenye Kata ya Msimbati kikiwamo Kijiji cha Madimba,
zitakarabatiwa na mwekezaji huyo ikiwa ni sehemu ya mpango wa wananchi
waishio maeneo ya mradi kunufaika na uwekezaji.
Hata
hivyo, habari nyingine zinaeleza kuwa ulinzi umeimarishwa katika eneo
hilo la mradi ili kuhakikisha hali ya usalama inaendelea kuwapo.
Mwananchi
No comments:
Post a Comment