Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mke wake Mama Salma Kikwete wakimpa
pole Bw. Yusuf Abdallah ambaye ni mmoja wa majeruhi walionusurika katika jengo
lililoporomoka katikati ya jiji Ijumaa iliyopita na kusababisha vifo vya watu
25, katika wodi ya Sewa Haji ya Taasisi ya Mifupa ya MOI katika Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam. kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa), Mhe. Hawa Ghasia.
Jakaya Mrisho Kikwete na Mke wake Mama Salma Kikwete wakiwa katika wodi ya Sewa haji ya Taasisi ya Mifupa ya MOI katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam leo Machi 31, 2013 wakimjulia hali na kumpa pole Bw. Selemani Saidi, mmoja wa majeruhi walionusurika katika jengo lililoporomoka katikati ya jiji Ijumaa iliyopita na kusababisha vifo vya watu 25 Kushoto mwenye suti nyeusi ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Raymond Mushi Kulia ni Daktari C.N. Mcharo wa taasisi ya Mifupa ya Moi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mke wake Mama Salma Kikwete wakiwa katika
wodi ya Sewa haji ya Taasisi ya Mifupa ya MOI katika Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili jijini Dar es salaam leo Machi 31, 2013 wakimjulia hali na kumpa pole
kijana Baqir Dhamji, mmoja wa majeruhi walionusurika katika jengo
lililoporomoka katikati ya jiji Ijumaa iliyopita na kusababisha vifo vya watu
25. Kulia ni Daktari C.N. Mcharo wa taasisi ya Mifupa ya MOI.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mke wake Mama Salma Kikwete wakiwa
katika wodi ya Taasisi ya Mifupa ya MOI katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
jijini Dar es salaam wakimpa pole kijana Mohamed Ally Dhamji ambaye ni miongoni
mwa majeruhi walionusurika katika jengo lililoporomoka katikati ya jiji Ijumaa
iliyopita na kusababisha vifo vya watu 25.PICHA NA IKULU.
No comments:
Post a Comment