HATUA ya vyombo vya habari kulivalia njuga suala la
kutekwa, kuteswa na kuumizwa kwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Absalom
Kibanda haiwafurahishi watendaji wa serikali.
Vyombo kadhaa
vya habari yakiwemo magazeti, vimekuwa na habari, makala na maoni mfululizo
kuisukuma serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi iwasake na kuwafikisha
mahakamani wahusika wa tukio la Kibanda ambaye pia ni Mhariri Mtendaji wa
Kampuni ya New Habari (2006).
Katika habari
hizo, vyombo hivyo vinaeleza kushangazwa na kitendo cha Jeshi la Polisi
kushughulikia matukio mepesi haraka na kwa kutumia nguvu nyingi, huku sakata la
Kibanda na lile la Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk. Stephen Ulimboka
uchunguzi wake ukidorora.
Msukumo huo wa
vyombo vya habari kuvisakama vyombo vya dola na baadhi ya vigogo serikali
kuhusika na matukio hayo umepokelewa kwa mtazamo hasi.
Habari za
uhakika zinasema kuwa vigogo kadhaa wameanza kuhaha kupanga mikakati ya kuvizima
vyombo hivyo, hususani magazeti ya Tanzania Daima na Mtanzania ambayo yamekuwa
mstari wa mbele kuandika sakata hilo.
No comments:
Post a Comment