Na Kemeli Arap Kemei, Father Kidevu Blog-Nairobi
Wananchi
wa Kenya wakiwa katika mitaa mbalimbali wakishangilia kwa furaha ushindi
wa Mgombea Urais wa kwa tiketi ya TNA Uhuru Kenyatta.
Kenyatta ameshinda Uchaguzi Mkuu wa Kenya kwa kura 6,173,433 dhidi ya mpinzani wake Raila Odinga aliyekuwa na kura 5, 340,546 ikiwa ni tofauti ya kura 832,887 .
Jumla ya
kura zote zilizopigwa na kuhesabiwa kwa nafasi ya Urais ni kura 12,338,
667 kutoka katika majimbo yote ya Uchaguzi 291 huku kura zilizoharibika
zikiwa 108975 na kura halali zikibaki 12,222,980.
Wakenya
wapo katika mitaa mbalimbali na vitongoji vya Nchi hiyo wakishangulia
ushindi huo, na wakati huu Maandalizi katika eneo la Bomas kwaajili ya
kutangaza rasmi matokeo hayo yanaendelea ambapo Mwenyrekiti wa Tume ya
Uchaguzi ya Kenya IEBC anataraji kumtangaza Rasmi Uhuru Kenyatta kama
Mshindi wa Urais.
Hii ndio
hali halisi ya hivi sasa nchini Kenya lakini kubwa zaidi la kuwapongeza
wakenya wote ni hali ya amani iliyopo katikia miji mbalimbali. Pia
Wagombea ambao wamekubali matokeo hayo huku wengine wakitangaza tangu
jana kukubali kushindwa na kuungana katika kuijenga Kenya moja iliyo na
amani na utulivu.
No comments:
Post a Comment