UKATILI wa kusikitisha! Watoto watatu wa famila moja, wameuawa kikatili kwa kunyongwa huku mama yao akishuhudia. Miili yao pamoja na mama yao akiwa hai, wakatumbukizwa katika kisima cha maji. Baba wa watoto hao, Justine Albert (24) anatuhumiwa kufanya unyama huo.
Kabla ya
mauaji hayo, inadaiwa baba huyo alimfunga kamba mkewe na kumziba mdomo
kwa kitambaa ili asipige kelele, kisha akaanza kuwanyonga watoto wake
wote watatu kwa zamu.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari, alisema mauaji hayo ya
kikatili yalifanyika juzi saa 11:30 alfajiri katika Kijiji cha Majimoto,
Bonde la Ziwa Rukwa wilayani Mlele mkoani humo.
Kwa
mujibu wa Kamanda Kidavashari, kisa cha kufanya mauaji hayo ni mzozo wa
mtuhumiwa na mkewe, Jacqueline Luvika (21), kwamba baadhi ya watoto hao
mama huyo kazaa na jirani yao.
No comments:
Post a Comment