Wema Sepetu akiwa na pete aliyovishwa na Dimaond.
Na Gladness Mallya
KATIKA
ulimwengu huu kuna mambo mengi yanayofurahisha. Yapo pia
yanayosikitisha na utapeli katika uhusiano wa kimapenzi umetamalaki.
Nimeanza
na utangulizi huo nikiwa na maana kuwa katika jamii inayotuzunguka
inabidi mtu uwe makini lasivyo utajikuta kwenye wakati mgumu hasa kwa
wasichana wanaohitaji kuolewa.Kumekuwa na tabia ya baadhi ya wanaume kuwarubuni wanawake wakiwadanganya kuwa watawaoa, ahadi ambazo hazitimii…
Kumekuwa
na tabia ya baadhi ya wanaume kuwarubuni wanawake wakiwadanganya kuwa
watawaoa, ahadi ambazo hazitimii kwani mapenzi yao huwa yanaishia njiani
kabla hawajatimiza lengo na kuwaacha wenzao katika maumivu makali.
Ni staa mkubwa wa filamu za Kibongo
ambaye alichumbiwa kwa muda mrefu na jamaa aliyekuwa mmoja wa kundi la
kitambo la Bongo Fleva kutoka Tanga la TNG, Malick Bandawe.
Rose amekuwa akiahidi kila kukicha kuwa
harusi yake iko mbioni lakini umepita muda mrefu hakuna ndoa wala nini
na badala yake wamebaki kuishi pamoja kama mume na mke.
Ni mkata mayenu kiraka wa Bendi ya
Extra Bongo ‘Wazee wa Kizigo Staili’. Alivishwa pete ya uchumba miaka
miwili iliyopita na mume wa mtu anayejulikana kwa jina moja la Ally
lakini mpaka sasa ndoa imebaki ndotoni.
Otilia na mchumba wake huyo wanaishi pamoja kama mume na mke na suala la ndoa bado wanajiandaa.
Ni mnenguaji bei mbaya wa Bendi ya FM
Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’. Alivishwa pete ya uchumba zaidi ya miaka
miwili iliyopita na aliyekuwa rapa wa bendi hiyo, Aimerichard Mwamba
‘G-Seven’ ambaye kwa sasa amehamishia makazi yake Nairobi, Kenya na
kumwacha Suzy Bongo.
G-Seven alimposa Suzy pamoja na
kumvisha pete ambapo uchumba wao ulidumu kwa muda mrefu kabla ya hivi
karibuni bishosti huyo kuweka wazi kuwa ameamua kuachana naye kwa sababu
aligundua kuwa siyo mwaminifu.
Ni Miss Ruvuma 2006. Anasaka mkate wa
siku kupitia filamu na muziki wa Bongo Fleva. Alivishwa pete ya uchumba
kitambo na kutolewa mahari na mwanaume jina kapuni lakini aliishia
kupewa mimba na kuzaa.
Baada ya kuzaa Isabela mpaka sasa
hajaolewa na amejaliwa kuwa na watoto wawili kila mmoja na baba yake
huku ikifahamika kuwa yupo kwenye uhusiano wa kimapenzi na mwanamuziki
Luteni Kalama.
Ni Miss Tanzania 2009 aliyevishwa pete
ya uchumba na msanii wa filamu za Kibongo, Kennedy Victor ‘Kenny’.
Walipanga kufunga pingu za maisha mwezi Juni, mwaka jana lakini hadi
unaposoma hapa hakuna chochote zaidi kujaliwa mtoto mmoja wa kiume.
Ni mwanadada mrembo kutoka kiwanda cha
filamu za Kibongo. alivishwa pete ya uchumba na mwanamuziki wa Bongo
Fleva, Nasib Abdul ‘Diamond Platnumz’ lakini mapenzi yao hayakufika
mbali, waliishia kuachana na mambo ya ndoa yakaishia hapo huku bidada
akiendelea kujikusanyia pete za uchumba kabatini kwake baada ya ile ya
Yusuf Jumbe.
Ni staa wa filamu za Kibongo ambaye kwa
muda mrefu amechumbiwa na jamaa mmoja aitwaye Dick. Uchumba wao una
zaidi ya miaka miwili lakini ndoa imekuwa ni kitendawili huku wakijaliwa
mtoto mmoja wa kiume aitwaye Terry.
Ni
staa wa filamu za Kibongo ambaye aliwahi kudaiwa kuvishwa pete ya
uchumba na mwigizaji mwenzake aitwaye Godfrey Kusila kabla ya uchumba
kuvunjika na penzi kuhamia kwa mwanamuziki Elibariki Emmanuel ‘Ney wa
Mitego’. Hata hivyo, kwa Ney wa Mitego napo uchumba uliota mbawa pamoja
na kuwa na mbwembwe nyingi.
NA GPL
No comments:
Post a Comment