Wakati
mwingine si kitu rahisi kupima ushawishi lakini tutaangalia ni wazo
mawazo gani ya mtu, mifano gani ya mtu, kipaji gani cha mtu na ugunduzi
gani wa mtu uliobadilisha jambo katika nchi yetu. Hawa ndio mastaa 20 wa
burudani, michezo na urembo Tanzania wenye ushawishi mkubwa zaidi,.
1. Wema Sepetu
Well,
well, well kunaweza kukawa na mjadala mrefu sana hapa wa kwanini mrembo
huyu akamate nafasi ya kwanza wakati kila kukicha amekuwa akigonga
vichwa vya habari kwa scandals kibao. Hiyo ni kweli lakini ukiugeuza
umaarufu huo wa Wema na kuupeleka katika muktadha wa biashara na jinsi
anavyokubalika, hakuna anayemfikia Wema. Wema ni brand inayouzika
kirahisi. Kuandikwa mara kwa mara kwenye magazeti ya udaku ambapo mara
nyingi si kwa kupenda yeye, kumemfanya Wema awe dhahabu inayotamaniwa
kushikwa na kila mtu. Habari za Wema hapa Bongo5 zimekuwa zikipata hits
(kusomwa zaidi) kuliko habari yoyote ya staa yoyote yule unayemjua hapa
Tanzania.
Iwe picha
akiwa kwa daktari aking’olewa jino, picha za mtindo mpya wa nywele,
tattoo aliyojichora, picha za mbwa wake, Gucci na Vanny, picha
zinamuonesha akiwa na shoga zake Kajala na wengine, kila kitu kuhusu
Wema kinavutia attention ya watu. Story za Wema husomwa zaidi na kupata
comments nyingi kuliko za wengine wote.
Kama leo hii
Wema akisema aanzishe bidhaa yoyote inayowalenga vijana, haitachukua
muda kushika na kutafutwa kama njugu. Wema ni show stopper! Kama
akiingia ukumbini kwenye shughuli, shughuli hiyo husimama kwa muda
kutokana na watu kugeuka kutaka kumwangalia kwa uzuri zaidi wakati
akielekea sehemu ya kukaa. Kutoka kuwa Miss Tanzania na sasa akiwa
muigizaji wa orodha A Tanzania, CEO wa kampuni ya filamu, Endless Fame
Films, Wema Sepetu ni mwanamke mwenye ushawishi mkubwa.
2. Diamond
Ni msanii
gani Tanzania ambaye nyimbo zake zinahit mtaani bila hata kupigwa
redioni? Bila shaka umeshasikia nyimbo nyingi za Diamond mtaani siku za
hivi karibuni ukiwemo UKIMWONA na ukajiuliza iweje unahit wakati
haujaachiwa rasmi? Muziki wa Diamond umekuwa ukitumika kama tulizo la
wanyonge walio kwenye mahaba mazito. Kuanzia Mbagala, Nitarejea, Lala
Salama, Mawazo ama Nataka Kulewa, zote zimekuwa zikitumiwa na watu wa
rika mbalimbali, madaraja tofauti ya kiuchumi, wanawake kwa wanaume na
watoto kama burudisho la roho zao. Diamond Platnumz hi hitmaker na
haoneshi dalili za kupunguza kasi.
Diamond
ndiye msanii anayefanya show nyingi zaidi ndani na nje ya Tanzania na
kwa kulipwa gharama kubwa kuliko msanii mwingine yeyote muda huu. Hujaza
kumbi kubwa za starehe yeye mwenyewe bila backup ya msanii mwingine na
kuwaacha wasichana wakibubujikwa na machozi ya furaha na kutamani walau
kukishika tu kifua chake kilichoanza kupasuka kwa mazoezi.
Kwa
mujibu wa kampuni ya Push Mobile, Diamond ambaye jina lake halisi ni
Nasib ndiye msanii anayeuza zaidi nyimbo zake kama miito ya simu (RBT).
Pamoja na
kuzungukwa na scandal kibao kuhusu wanawake, Diamond ni kijana mwenye
mawazo pevu na ya kiutuuzima. Akiwa ametoka kwenye familia duni na
kupata misukosuko mingi ikiwemo kutengwa na baba yake na kulelewa zaidi
na mama yake, Diamond amekuwa akitoa ushauri na kuwapa moyo watafutaji
wa maisha wasikate tamaa. Hupenda kutoa ushauri kwa vijana wenzie
kuhusiana na umuhimu wa kujituma, kuchapa kazi, kumuabudu mwenyezi Mungu
na kutokata tamaa.
Katika
kuhakikisha kuwa anaitolea pia jamii, hivi karibuni alitangaza kuwa na
nia ya kujenga msikiti. Ni kwa sababu zipi kijana huyu asiwe na
ushawishi?
3. Millard Ayo
Japo si
kituo chake cha kwanza kuanza kazi, jina la Millard lilianza kufahamika
nchini kupitia kipindi cha Milazo 101 cha Radio One. Sauti yake yenye
mamlaka na ubunifu hewani, ulikifanya kipindi hicho kuwa maarufu kuliko
vingine vya burudani katika radio hiyo inayomilikiwa na kampuni ya IPP.
Kuondoka
kwake Radio One kulikuwa ni pigo kubwa lakini lenye neema kwa Clouds FM.
Alihamia Clouds FM na kuanzisha kipindi kipya kiitwacho Amplifanya
ambacho kilichukua nafasi ya kipindi cha nyimbo za kiafrika, Bambataa.
Haikuchukua muda kipindi cha Amplifanya kikawa miongoni mwa vipindi bora
kabisa Clouds FM.
Leo hii
Millard ni miongoni mwa watangazaji bora Tanzania na wanaosikilizwa
zaidi. Si maarufu tu redioni bali pia ndiye mtangazaji wa Tanzania
mwenye mashabiki wengi zaidi kwenye mitandao ya kijamii. Ana zaidi ya
followers 40,000 kwenye Twitter huku Facebook akiwa na likes zaidi ya
90,000.
Umaarufu
wake kwenye mitandao ya kijamii umemfanya ageuke brand na kuyavutia
makampuni makubwa kama CRDB Bank, Fast Jet na mengine kudhamini kile
anachotweet. Tweets zake tu zinamuingizia fedha huku akimiliki pia
website yake binafsi yenye wasomaji lukuki. Pamoja na kupata mafanikio
hayo, Millard ameendelea kuwa mchapakazi, simple, mtu anayejituma
kutafuta habari hata sehemu za mbali kabisa, mcheshi na mtu wa watu.
4. Nancy Sumari
Nancy Sumari
ni msichana mrembo, mpole na mcheshi. Ndiye Miss Tanzania wa kwanza
aliyewahi kufika mbali zaidi kwenye shindano la Miss World ambapo mwaka
2005 alifanikiwa kuwa Miss World Africa.
Kwa sasa
Nancy ambaye ni mama wa mtoto mmoja wa kike, ni mwanafunzi katika Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam na anasoma Shahada ya Biashara. Pia ni
mjasiriamali na anafanya kazi zake na jamii zikiwemo kuwahamasisha
watoto wa kike kujitambua na kuthubutu, ili kutimiza ndoto zao.
Katika
harakati zake za kuhakikisha wasichana wa Tanzania wanatambua haki zao,
anaendesha programu iitwayo Mentorship, ambayo inazunguka kwenye shule
mbalimbali za serikali za wasichana nchini, na kuzungumza nao kuhusu
maisha. “Kwenye programu hiyo, tunabadilishana mawazo na wanafunzi na
wao wanazungumza changamoto wanazokutana nazo na kupeana mawazo jinsi ya
kufanya kwani nawaambia wakiamua kuthubutu wanaweza kufanikiwa, na
wanaonesha wanaweza,”Nancy aliliambia gazeti la Habari Leo hivi
karibuni.
Pamoja na
hayo pia Nancy anashirikiana na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), kwenye
kampeni ya kujenga mabweni ya wasichana kwenye shule za sekondari za
serikali nchini, ili kuhakikisha watoto wa kike wanapata elimu.
Hivi karibuni
alizindua kitabu chake kwaajili ya watoto ‘Nyota Yako’ kinachomlenga
mtoto wa kike kuona jinsi wanawake wengine walivyofanikiwa licha ya
kupitia changamoto mbalimbali.
“Ninaamini
kitabu kitasomwa na wengi ndio maana nikaamua ujumbe wangu niufikishe
kwa njia hii, watasoma watoto wetu hata wajukuu kitajenga kitu kwenye
akili ya mtoto na wakisoma shuhuda za hao waliofanikiwa nao watathubutu”
aliliambia Habari Leo. Tanzania itegemee mengi makubwa kutoka kwa
mrembo huyu.
5. Ambwene Yesaya aka AY
Safari ya AY
mpaka kuja kuwa nyota anayefahamika Afrika nzima na sehemu zingine
duniani haikuwa rahisi. Amepitia mengi. Aliwahi kusema kuwa kabla ya
kufahamika Afrika Mashariki, alikuwa akienda Kampala na Nairobi kufanya
show za bure ili tu kukuza jina lake, jitihada ambazo zilizaa matunda.
AY ni msanii smart, mbunifu, risk taker na anayeijua biashara ya muziki.
Ni msanii
wa Tanzania anayefanya video za ghali zaidi ambapo mpaka sasa video
zake tatu, Speak With Your Body aliowashirikisha wamarekani Lamyia Good
na Romeo, Partyzone na Money zilimgharimu zaidi ya dola 70,000 kwa
pamoja kuzikamilisha. Video zake zimekuwa zikichezwa kwenye vituo
vikubwa vya runinga duniani.
Mwaka
jana alifanikiwa kuandika historia kwa kushinda tuzo za Channel O katika
kipengele cha video bora ya mwaka ya Afrika Mashariki kwa wimbo wake I
don’t Wanna Be Alone aliowashirikisha Sauti Sol wa Kenya. Umaarufu na
busara zake ziliivutia kampuni ya simu ya Airtel mwaka jana na kumteua
kuwa balozi wake. Kwa sasa ni mwenyekiti mtendaji wa kampuni ya
burudani, Unity Entertainment, anajihusisha na biashara za nguo,
mwanzilishi wa kipindi cha televisheni cha Mkasi na biashara zingine.
Akiwa na
followers zaidi ya 40,000 kwenye Twitter, mwaka huu AY amekuwa msanii wa
kwanza wa Tanzania kupata alama ya tick ya blue ya verification kwenye
mtandao huo. Ni watu watano tu nchini wana alama hiyo.
6. Hasheem Thabeet
Hasheem
Thabeet ni mtanzania wa kwanza kucheza kwenye ligi ya mpira wa kikapu wa
kulipwa nchini Marekani, NBA. Akiwa na urefu wa 7 ft 3 Hasheem ndiye
mchezaji mrefu zaidi kwenye ligi hiyo. Anacheza timu ya Oklahoma City
Thunder kwa mshahara wa dola milioni 5.128 kwa mwaka.
Pamoja na
kuwa Marekani muda mwingi, Hasheem hasahau ya nyumbani na hupenda sana
kuongelea wasanii wa Bongo Flava kama alivyoandika.
“Mwaka
2000 mpaka mwaka 2005 Juma Nature alikuwemo katika kila nyimbo ambayo
ilikuwa hit ndani ya bongo. kubali au kataa. #fact.”
Akitumia
Twitter, Hasheem anajulikana kwa jinsi anavyopenda kuandika ujumbe wa
matumaini. Hizi ni tweets 5 zenye ujumbe utiao matumaini alizoandika
hivi karibuni.
No matter
what u go thru in life there is no need of gettin angry with god and
reflect bitterness to people around u. #havefaith.
The wise
ones speak b’se they have something to say… fools speaks b’se they have
to say somethin. thik before u speak. #liveandlearn.
Everything can change in a blink of an eye… but dont worry; god never blinks. #believe #havefaith
Life aint about how hard u can hit… it’s about how hard u can get hit and still move forward.
Envy is a waste of time… accept what you already have, not what u need.
7. Flaviana Matata
Flavy ni
mwanamitindo wa kimataifa aliyehamishia makazi yake nchini Marekani.
Amefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika fani hiyo kwa kushiriki kwenye
fashion show kubwa dunia, kufanya matangazo ya brand kubwa pamoja na
kuhusishwa kwenye majarida ya kimataifa.
Hivi karibuni Matata alishiriki katika kampeni za matangazo makubwa ya makampuni ya nguo ya DIESELna EDUN.
Kampeni
ya DIESEL + EDUN ilianzishwa mwaka jana mwezi wa kwanza ambapo
muanzilishi wa kampuni ya DIESEL – Renzo Rosso – na waanzalishi wa
kampuni ya EDUN – Ali Hewson na Bono walisafiri hadi nchi za Uganda na
Mali na kukutana na wakulima wa pamba barani Africa.
Waliingia
makubaliano ya kutengeneza nguo maalum zitakazotokana na pamba ya
wakulima hawa wa Afrika na hivyo kuwanufaisha moja kwa moja. Hivyo basi
nguo hizi zinatangazwa kama kampeni ili kunufaisha bara la Afrika.
Nguo hizo
zitaanza kupatikana mwanzoni mwa mwezi wa tatu katika maduka mbalimbali
nchini Marekani na duniani. Pia nguo za DIESEL + EDUN zitauzwa kupitia
mitandao mbalimbali.
Flaviana
ambaye aliwahi kuwa Miss Universe Tanzania 2007 anabaki kuwa
mwanamitindo pekee kutoka bara la Africa katika kushiriki katika kampeni
za nguo hizo.
Alianzisha
taasisi ya Flaviana Matata Foundation inayohusika kuwasaidia wasichana
kupata karo ya shule, sare na mahitaji mengine muhimu. Pia hutoa mafunzo
na misaada kwa wanawake ili waanzishe miradi mbalimbali ili kujiongezea
kipato.
8. Loveness Diva
Diva Love
Loveness ni mtangazaji maarufu zaidi wa vipindi vya usiku. Ujasiri wake
wa kuzungumza masuala ya mapenzi bila kificho umemtengenezea maisha ya
pande mbili, kupendwa sana na kuchukukiwa sana. Ana mashabiki wengi.
Mara
kadhaa kauli zake zimewahi kuleta mijadala mizito nchini lakini bado
kipindi chake cha Ala za Roho cha Clouds FM kimeendelea kuwa kipindi
chenye wasikilizaji wengi zaidi ukilinganisha na vipindi vingine vya
aina hiyo katika vituo mbalimbali vya radio nchini.
Diva pia hujihusisha na shughuli za kusaidia wasiojiweza kupitia mradi wake wa Diva Giving for Charity.
9. Masanja Mkandamizaji
Huenda
watu wengi wanaweza wakawa hawafahamu kwamba Masanja ndiye staa wa
Tanzania mwenye likes nyingi Facebook, 104,670 na zaidi. Masanja ni
miongoni mwa wachekeshaji wa kizazi kipya wenye mashabiki wengi zaidi.
Umaarufu wake umetokana na kipindi cha Ze Komedi kilichoanzisha EATV na
sasa kikiwa TBC 1. Pamoja na kuwa mchekeshaji, Masanja ni muimbaji wa
nyimbo za injili, mchungaji mtarajiwa na mambo mengine. Huzitumia
akaunti zake za mitandao ya kijamii kuchekesha na kuwafurahisha zaidi
followers wake na ni miongini mwa mastaa wanaopata comments nyingi zaidi
kila wawekapo status.
10. Mwana FA
Hamis Corlone
Mwinjuma aka Mwana FA ni rapper anayeaminika kuwa miongoni mwa
waandishi bora wa mashairi ya Hip Hop kuwahi kutokea katika muziki wa
kizazi kipya nchini Tanzania.
Jina lake
lilianza kuvuma mwaka 1998 alipotoa ngoma yake ‘Ingekuwa Vipi?’ akiwa
na Jay Mo na pia ‘Mabinti’ ambayo ilitayarishwa na Bonny Luv.
Mwaka
2003, ngoma yake ‘Alikufa Kwa Ngoma’ – ilimpa tuzo kama wimbo bora wa
Hip Hop wa mwaka kwenye Kili Music Awards. Mwana FA aliendeleza utemi
kwa kuachia hits kibao kama Unanitega, ‘Hawajui’ feat. Lady Jaydee,
Habari Ndio Hiyo akiwa AY, Bado Nipo Nipo, Unajijua Unanisikia, Yalaiti
na ngoma ya hivi karibuni Ameen.
Mwaka huu anasubiriwa kwa hamu kuachia ngoma yake mpya iitwayo Kama Zamani aliyowashirikisha Njenje.
Pamoja na
kufanya muziki, Mwana FA aliamua kwenda nchini Uingereza kuongeza shule
yake ambako alisoma shahada ya Finance katika chuo kikuu cha Coventry.
Ana
mipango pia ya kuendelea na masomo ya PhD siku za usoni. Kwa sasa
ameanzisha pia kampuni ya kusimamia wasanii iitwayo Lifeline Music Inc
ambayo tayari ina msanii mmoja aitwaye Maua Sama.
11. Salama Jabir
Salama ni
mhasisi wa kipindi cha Planet Bongo cha EATV ambacho enzi anakifanya
kilichangia ubora wa video za muziki wa Bongo Flava nchini kutokana na
kasumba yake ya kuzikosoa bila woga. Baada ya kuondoka EATV na East
Africa Radio, Salama alienda kusoma nchini Uingereza na kurudi kukaa nje
kwa muda na mambo ya habari. Alikuja kurejea tena na kipindi cha Mkasi
kinachorushwa EATV na kukifanya kuwa kipindi bora kabisa cha mahojiano
nchini. Salama ni mcheshi, mtundu na anaufahamu mkubwa wa masuala ya
burudani. Namna ya uulizaji wake wa maswali hufanya vipindi vyake kuwa
na mvuto zaidi.
12. Fid Q
Fareed
Kubanda si rapper anayeheshimika tu kama mwandishi mkali wa mashairi,
bali pia anatambulika kwa kujihusisha kwake na shughuli za kijamii.
January
mwaka huu, Taasisi ya Under The Same Sun inayojihusisha na kutetea haki
ya watu wenye ulemavu wa ngozi, albino nchini, ilimtunuku ‘cheti cha
shukrani’ kwa mchango wake katika kampeni ya shirika hilo.
Alipata
cheti hicho baada ya mwaka jana kujumuika na taasisi hiyo katika ziara
yao ya kanda ya ziwa akiwa kama muelimishaji kwenye vita dhidi ya mauaji
ya ALBINO.
“Kujituma
kwenye uchapaji kazi na utaratibu wa kuwa na nidhamu kazini ni moja
kati ya vitu vilivyowafurahisha,” aliiambia Bongo5.
Pia mwaka jana Fid alikuwa akiendesha darasa la hip hop la hiari jijini Dar es Salaam.
Akielezea
madhumuni yake, Fid alisema, “Kwa haraka haraka hip hop darasa maudhui
yake ni kuwafundisha vijana wawe na positive thinking na attitude kwa
jamii, yaani wawe na fikira zilizopo katika mstari ulio sahihi na hata
kitabia, kwahiyo tunawajenga hivyo kupitia muziki wa hiphop.”
13. Lady Jaydee
Mpaka
sasa Lady Jaydee ana albam tano na hivi mwezi ujao ataachia albam ya
sita aliyoipa jina NOTHING BUT THE TRUTH. Ndiye msanii wa kike Tanzania
anayeheshimika na mwenye mafanikio zaidi. Jaydee ni mjasiriamali ambaye
hutumia pia kipato anachokipata kwenye biashara zake kusaidia watu
wanaohitaji msaada hususan watoto yatima wanaolelewa kwenye vituo
maalum.
Mwaka huu
Lady Jaydee ambaye ana likes zaidi ya 47,000 Facebook na followers
zaidi ya 22,000 Twitter, aliweka historia kwa kufanikisha safari ya
kuupanda mlima Kilimanjaro na kuwa msanii wa kwanza wa kike nchini
kufanya hivyo.
13. Jacob Stephen
Jacob
maarufu kama JB, ni muigizaji ambaye wachambuzi wa filamu za Tanzania
wanadai kuwa msanii pekee wa kiume anayeweza kufikia mafanikio ya
marehemu Steven Kanumba. Ni muigizaji wa kiume anayependwa zaidi kwa
sasa na filamu zake zimekuwa kivutio kwa watu wengi wa kila rika. Ana
uzoefu wa zaidi ya miaka 14 kwenye sanaa ya uigizaji.
Kwa sasa
anamiliki kampuni ya filamu iitwayo Jerusalem ambayo imesaidia kuwaibua
wasanii wengine akiwemo Rose Ndauka, Elizabeth Kiyumba ’Nikita’ na
wengine.Pamoja na kuwa muigizaji pia JB ni mhubiri wa masuala ya dini.
15. Jokate Mwegelo
Jokate ni
mtangazaji wa TV (Channel 0), muigizaji wa filamu, mwanamuziki na
mjasiriamali. Umaarufu wake ulianza aliposhiriki shidano la Miss
Tanzania mwaka 2006 na kukamata nafasi ya pili na kupata ubalozi wa
Redd’s na gazeti la The Citizen.
Jokate
amewahi pia kushinda tuzo za ZIFF kama muigizaji bora wa kike. Pamoja na
hivyo hujihusisha na muziki pia ambapo amewahi kushirikishwa na AY
kwenye wimbo Kings and Queens na hivi karibuni amesikika kwenye wimbo wa
Lucci, Water up.
Hivi
karibuni alijiingiza kwenye biashara ya ubunifu wa mitindo kwa kuanzisha
kampuni na brand ya Kidoti ambayo hubuni nguo pamoja na kutengeneza
nywele za aina mbambali zinazopatikana nchini.
16. Vanessa Mdee
Vanessa
ni mtangazaji mahiri wa MTV Base na Choice FM. Uwezo wake mkubwa wa
kutangaza, maarifa kuhusu burudani na mambo mengine vimemfanya awe
miongoni mwa watangazaji wa kike wakali zaidi barani Afrika na wenye
mashabiki lukuki.
Vanessa
amefanikiwa pia kwenye muziki ambapoi alimake headline sana
aliposhirikishwa na Ommy Dimpoz kwenye Me and You iliyotoka mwishoni mwa
mwaka jana. Sauti tamu kwenye chorus hiyo iliwashtua wengi kwakuwa
alikuwa akijulikana kama mtangazaji tu.
January
mwaka huu aliachia single yake ya kwanza Closer. Ngoma hiyo ilipokelewa
vizuri na mashabiki wa muziki na miongoni mwa nyimbo zilizopata
downloads nyingi zaidi mtandaoni. Na sasa ametajwa kuwania tuzo za Kili
kama msanii bora anayechipukia huku wimbo Me and You alioshirikishwa na
Ommy ukitajwa pia kwenye vipengele kibao. Ashafanikiwa kushare stage
moja na wasanii wa kimataifa wakiwemo Mi Casa Music wa Afrika Kusini.
17. Rita Paulsen
Maadam
Rita anafahamika zaidi Facebook kwa wafuasi wake zaidi ya 25,000 kama
mwanamke mwenye ushauri muhimu kuhusu maisha. Ni mwanzilishi wa shindano
kubwa la kusaka vipaji vya kuimba nchini, Bongo Star Search ambalo
limefanikiwa kutoa vipaji vingi na kwa kuwazawadia washindi vitita vya
pesa. Ni mcheshi, mrembo na ambaye siku zote hupenda kuwapa moyo hata
wale ambao uwezo wao ni mdogo.
18. Profesa Jay
Profesa Jay
ni miongoni mwa wasanii waliyoifanya Bongo Flava ipate mafanikio. Akiwa
na albam nne mpaka sasa, Machozi Jasho na Damu 2001, Mapinduzi Halisi
2003, J.O.S.E.P.H 2006 na Aluta Continua 2007, Prof amewahi kushinda
zaidi ya tuzo 6 mbalimbali zikiwemo za Kili. Mpaka sasa hits zake
zikiwemo Bongo Dar es Salaam, Jina Langu, Zali la Mentali, Nikusaidije
na zingine zinaendelea kutoa burudani isiyo na kifani katika masikio ya
mashabiki wake.
19. Dj Fetty
Fetty aka
Fetilicious ni Dj pekee wa kike wa Tanzania aliyefanikiwa hadi mwaka
jana kupata shavu la kwenda kupiga muziki kwenye jumba la Big Brother
Africa. Ni msichana mrembo, anayejiamini na machachari hewani huku akiwa
na fanbase ya nguvu. Ana likes zaidi ya 57,000 kwenye Facebook na
followers zaidi ya 25,000 kwenye Twitter. Pamoja na kuwa mtangazaji wa
kipindi pendwa cha XXL, Clouds FM, Fetty ni dj kwenye club ya
Ambassodors Lounge jijini Dar.
20. Mzee Majuto
Kwa wengi
King Majuto ni mchekeshaji bora zaidi nchini kuliko wachekeshaji wote.
Ni comedian wa kuzaliwa ambaye sura yake tu huwavunja mbavu watu. Filamu
zake zinauzika zaidi huku akiwa na mashabiki kibao katika nchi zingine
za Afrika zinazozungumza Kiswahili. Umaarufu wake umemfanya apate deals
za kufanya matangazo mbalimbali yakiwemo ya Airtel na Azam.
“Jina la
King Majuto limeweza kuwa maarufu zaidi kwake, kutokana na kazi yake ya
uigizaji katika filamu za vichekesho, mafanikio yake katika uigizaji
yamefanya waigizaji chipukizi kutamani kumshirikisha msanii huyo mkongwe
na wengine kujifunza kupitia kwake. Wapo wasanii chipukizi ambao
wanatamani kufika kiwango alichofikia King Majuto, akitamba katika fani
kwa zaidi ya miongo mitatu sasa bila kuchuja wala kutetereka.”
source:bongo5. (43)
No comments:
Post a Comment