MBUNGE wa
Nkasi Kaskazini, Ali Kessy Mohammed (CCM) ameishauri Serikali kuachana
na kuhamasisha kilimo cha tumbaku kwa vile kinasababisha magonjwa ya
kansa; badala yake iruhusu kilimo cha bangi.
Akiuliza
swali la nyongeza jana bungeni, Kessy alisema zao la tumbaku linapingwa
kote duniani; hivyo sio vyema kwa Serikali kuendelea kuhamasisha kilimo
chake na ni vyema ikaruhusu bangi kwa vile ina uwezo wa kuliletea taifa
fedha za kigeni.
“Kwa nini
tusiruhusu kilimo cha bangi kuliletea taifa fedha za kigeni badala ya
kuhamasisha kilimo cha tumbaku?” Alihoji mbunge huyo na kusababisha
wabunge kulipuka kwa kicheko.
Katika
majibu ya Serikali, Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Adam
Malima alisema ni kweli kwamba zao la bangi limesharuhusiwa katika
baadhi ya nchi hapa duniani.
Lakini
alisema kwa hapa nchini hawawezi kuruhusu kilimo cha zao hilo kwa sababu
bangi bado inachukuliwa kama ni zao la dawa za kulevya na linapingwa
katika baadhi ya nchi.
“Siku
tukijiridhisha kuwa bangi imepata uhalali duniani kote na imekubaliwa
kulimwa na sisi tutaelekea kwenye kilimo cha zao hilo lakini kwa sasa
hatukiruhusu,” alisema Malima.
Alisema
katika kipindi hiki sio wakati wa kupuuza kilimo cha tumbaku kwa vile
ndilo zao pekee ambalo kwa sasa linalipatia taifa fedha nyingi za
kigeni.
No comments:
Post a Comment