Arusha,Tanzania
MAMBO
yamezidi kumwendea kombo Mbunge wa Arusha Mjini, (Chadema) Godbless Lema
baada ya Jeshi la Polisi kutangaza rasmi kwamba itamfikisha Mahakamani,
siku ya Juma tatu.
Mwanadishi wa Habarimpya.commjini Arusha anasema kwamba, Kamanda wa Polisi Mkoa wa ArushaLiberatus
Sabas amema kwamba Mbunge huyo hawezi kuachilia huru kwa sababu
mashtaka dhidi yake yameshakamilika na atafikishwa Mahakamani siku ya
Juma tatau.
"Hatuwezi kumwachia kwa sababu anatarajia kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili"alisema Sabas.
Wakati
Kamanda huyo akitoa msimamo huo, taarifa za ndani ya Jeshi hilo
zinaeleza kwamba Mbunge huyo amehojiwa kwa zaidi ya saa nane sasa na
bado yuko katika chumba maalum kwa mahojiano zaidi na maofsa wa Polisi
huku akitakiwa kuonyesha ujumbe mfupi wa vitisho aliyodaiwa kuwa
ametumiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa Mulongo.
Katika
hatua nyingine Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Arusha, kimekuwa
na kikao kirefu kinachoongozwa na Mkuu wa Mkoa Mulongo na kwamba ajenda
kubwa inayojadiliwa ni tukio zima la vurugu zilizotokea katika Chuo cha
Uhasibu mkoani humo. Lema
alikamatwa usiku wa kuamkia leo baada ya Askari wa Jeshi la Polisi
kumfuata nyumbani kwake na kuzingira nyumba yake kabla ya zoezi la
kumchomoa ndani ya nyumba hiyo kufanyika.
Mbune
huyo anatuhumiwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo kosa la kuchochea vurugu
katika chuo hicho baada ya kutokea mauaji ya Mwanafunzi Henry Koga aliye
uawa kwa kuchomwa kisu juzi akirejea chuoni hapo kutoka kwenye
matembezi yake, hata hivyo haijajulikana mara moja sababu za kuawa kwa
mwanafunzi huyo wala watuhumiwa hawajakamatwa.
No comments:
Post a Comment