Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, April 3, 2013

RIPOTI MAALUMU KUHUSU VURUGU ZA TUNDUMA ZILIZOSABABISHA MIPAKA KUFUNGWA KWA MUDA



Taarifa  kutoka Tunduma mkoani Mbeya zinadai  kuwa hali  si shwari katika eneo hilo kutokana na kuzuka kwa  vurugu kubwa zinazodaiwa kusababishwa na masuala ya  kiimani ya nani achinje kati ya mkristo na Muislam .

Mwandishi   wetu  kutoka Tunduma mkoani Mbeya  anaripoti kuwa  vurugu  hizo zimeanza  majira ya saa nne asubuhi  kwa makundi  ya vijana  kuandamana mitaani na kuvutana  kuhusu uamuzi  wa viongozi  wa dini ya kikristo Tunduma  kuandika barua kwa mkuu  wa wilaya  kutaka  kuruhusiwa kuchinja  wakati wa pasaka.

Ripota  wetu anaripoti   kuwa kabla ya  ijumaa kuu  viongozi hao  wa dini ya Kikristo  walikutana na mkuu  wa  wilaya  ya Momba Abuud Saibea ambae  aliwataka kuwasilisha barua rasmi ya  kutaka  kibali  cha  kuchinja .

Hata hivyo inaelezwa  kuwa  vurugu  hizo za  leo zina mikanganyiko  mingi  kwani  wanaoshiriki katika  vurugu  hizo ni vijana  wapiga debe .....

Vurugu za  uchinjaji  zilifanyika  siku ya Pasaka  na hazikuwa na mvutano  kwa sababu wakristo  walichinja katika bucha zao na  waislamu nao  walichinja katika mabucha yao ....

Cha kushangaza leo ni baada ya  kuibuka  kundi  la  vijana  wanaofanya kazi katika stendi na vijiwe mbali mbali ambao  ndio walioanzisha  vurugu kiasi cha  polisi  kuingilia kati kwa kutumia mabomu ya machozi na kuwatawanya  wananchi  waliokuwa wamekusanyika maeneo mbali mbali .

Kutokana na vurugu  hizo mpaka  wa Tunduma  ambao unaingia nchi  za kusini  mwa Tanzania  ulifungwa  pamoja na magari yaliyokuwa yakitoka  Sumbawanga  pia  yalizuiwa  kuendelea na  safari hadi hali  hiyo  ilipotulia mida ya saa 8 mchana baada ya kamanda wa polisi wa mkoa  wa Mbeya  Diwani Athuman  kufika  eneo hilo.

1 comment:

  1. JAMANI HIVI SIKU HIZI KUNA UIKRISTO MPYA UNAORUHUSU KUCHINJA?

    MBONA ZAMANI WAIKRISTO WALIKUWA WANAWATAFUTA WAISLAM ILI WAWACHINJIE ?

    AU UKOSEFU WA AJIRA NA UGUMU WA MAISHA NDIO HUSABABISHA YOTE HAYA?

    ReplyDelete