Rais Kikwete na
Mkewe, Mama Salma Kikwete wakimpa pole Yusuph Abdallah katika Hospitali ya
Muhimbili walipotembelea majeruhi wa ajali ya kuporomoka jengo la ghorofa 16.
Picha na Muhidin Michuzi.
DAR ES
SALAAM.
FUNDI ujenzi,
Yusuph Abdallah ambaye amelazwa katika Taasisi ya Mifupa (Moi), ameeleza jinsi
alivyonusurika kifo baada ya jengo la ghorofa 16 kuporomoka Ijumaa
iliyopita.
Yusuph aliliambia Mwananchi akiwa wodini
kwamba kilichomponya ni neema za Mungu kwani kabla jengo hilo kuporomoka yeye
alikuwa ghorofa ya 15 kwenye jengo hilo katika Mtaa wa Indira Gandhi akiendelea
na ujenzi.
Alieleza kuwa hakuwa anafahamu
kinachoendelea, bali aliona ghafla jengo linaaanza kuporomoka, na baada ya hapo
hakufahamu zaidi kilichotokea hadi alipojikuta yuko
hospitalini.
“Kweli jengo lilipoanza kuporomoka
sikutambua nini kinachoendelea kwani nilipoteza fahamu na kujikuta nipo hapa
Muhimbili,” anasimulia Abdallah.
Alisema anahisi alipoanguka alifunikwa na
kifusi kilichomponda na kuvunja miguu yote.
Fundi huyo ambaye amefungwa plasta gumu
(P.O.P) miguu yote, alisema hakuweza kuona watu waliomwokoa.
Mwingine aokolewa na mkewe.
Mkazi wa Ubungo, Ally Mlela ambaye ni fundi
madirisha anasimulia jinsi mke wake alivyomwokoa katika ajali hiyo baada ya
kumtaka asiende kufanya kazi siku hiyo.
source http://www.mwananchi.co.tz
No comments:
Post a Comment