WANASIASA
wawili vijana ambao wamekuwa katika vita ya maneno na Naibu Katibu Mkuu
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Zitto Kabwe, kuhusu
madai waliyoyatoa kuwa anawindwa kuuawa, mwishoni mwa wiki iliyopita,
walijitokeza katika ofisi za Mtanzania Jumatano na kufunua siri na
matukio ya utesaji raia na mauaji ya kinyama ambayo yamekuwa yakitokea
kwa nyakati tofauti kwenye shughuli za kisiasa hapa nchini.
Wanasiasa hao, Juliana Shonza na Mtela Mwampamba, ambao wamefanya
mahojiano ya ana kwa ana na gazeti hili, walisema madai waliyoyatoa
awali kuwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willbrod Slaa, alitajwa na kada
wa chama hicho, Ben Saanane, kuwa alimtuma amuwekee sumu Zitto kwa lengo
la kumuua ni ya kweli kwa sababu walimkamata akiwa nayo na alikiri
jambo hilo na kumuomba msamaha Zitto kwa kitendo hicho.
No comments:
Post a Comment