INAUMA sana! Wakati
wazazi wakihenyeka na wakati mwingine kujinyima ili mabinti zao waweze
kupata elimu bora itakayowasaidia maishani mwao wapo wapuuzi
wanaokatisha jitihada hizo.
Mwanaume mmoja aitwaye Taliki
Juma mkazi wa Temeke – Wailesi jijini Dar es Salaam ameingia katika
dimbwi la AIBU baada ya kunaswa akiwa na mwanafunzi wa kidato cha pili
wakifanya mchezo mchafu.
Mbaya zaidi, bila haya wala
soni, Taliki alimwingiza binti huyo (jina na shule anayosoma
vinahifadhiwa kwa sababu za kimaadili) katika chumba anachoishi na
mwanamke anayedaiwa ni mke wake ambaye alikuwa safarini.
Chanzo
chetu cha habari kilipiga simu chumba cha habari na kueleza juu ya
tabia ya Taliki ya kwenda na denti huyo chumbani kwake tena akiwa kwenye
sare za shule.
Kikao cha
dharura kiliitishwa haraka baada ya sosi wetu kutoa maelekezo juu ya
habari hiyo ambapo kwa muda huo na foleni za jiji la Dar usafiri
uliopendekezwa ukawa ni pikipiki.
Haraka timu ya waandishi wetu ilielekea eneo la tukio lakini kwa bahati mbaya walikwama.
Taarifa
iliyopatikana kutoka kwa mtoa habari wetu ni kwamba, muda mfupi kabla
timu haijaingia eneo la tukio, Taliki alifanikiwa kukwepa mtego baada ya
kumuondoa denti huyo.
Wikiendi
iliyopita Mei 18, mwaka huu chanzo chetu kilekile kilipiga tena simu
kwa mwandishi yuleyule na kueleza kuwa jamaa kwa mara nyingine
amemwingiza yule denti chumbani kwake.
Timu A
iliondoka na kwenda moja kwa moja hadi eneo la tukio na kuliweka chini
ya uangalizi huku timu B ikielekea katika Kituo cha Polisi cha Wailesi
na kuomba ushirikiano wao.
Timu ya maaskari wa kituo hicho wakiwa tayari kwa lolote, waliungana na waandishi wetu kwenda eneo la tukio.
Waandishi
wetu, maaskari na wazee wachache wa mtaani hapo walivamia katika chumba
hicho na kufanikiwa kumnasa laivu Taliki akiwa na denti huyo kama
walivyozaliwa akimfanyisha mambo ya kikubwa muda ambao alitakiwa kuwa
darasani.
Binti
huyo ambaye alionekana kushtuka sana baada ya kukutwa chumbani hapo,
alieleza kuwa amekuwa katika uhusiano na Taliki kwa muda mrefu baada ya
kumrubuni kwa fedha na zawadi mbalimbali.
“Ni
kweli huyu hapa ni mpenzi wangu, huwa ananipa pesa. Nyumbani kwetu ni
Mwananyamala na nimetoka nyumbani nikienda tuisheni lakini Taliki
aliniambia nije kwake.
“Naombeni
mnisamehe jamani. Mama akijua atanipiga sana. Nisameheni tafadhali na
ninaahidi mbele yenu kuwa nitaachana kabisa na huyu mbaba
(Taliki),” alisema denti huyo.
Denti
huyo alitoa namba ya simu ya mama yake mzazi ambapo alipigiwa na kufika
eneo la tukio na kujionea jinsi mtoto wake anavyoharibiwa wakati yeye
akiwa kwenye juhudi za kumtengenezea maisha.
Mama wa binti huyo, hakuamini alichokiona na alijikuta akimwaga machozi muda wote, watu wazima wakapata kazi ya kumtuliza.
UPUUZI WA TALIKI
“Ni
kweli nakubali huyu ni mpenzi wangu na nipo naye muda mrefu ila
naombeni sana mnisamehe, kwa kweli ni shetani tu alinipitia (Mh! Huyu
shetani anasingiziwa mengi sana).
“Ndugu
zangu wakijua hili jambo watanitenga, naombeni muwe na roho ya huruma
(utadhani na yeye ana huruma), maisha yangu yataharibika (sijui alikuwa
anamtengenezea yule binti wa watu maisha?).”
Utetezi
wake haukusaidia na badala yake alifikishwa katika Kituo cha Polisi
Wailesi na kufunguliwa mashitaka katika Jalada nambaWS/RB/585/2013 –
KUFANYA MAPENZI NA MWANAFUNZI.
GPL
No comments:
Post a Comment