Kuna
tetesi kwamba Mwenyekiti wa Baraza la Mitihani la Taifa-NECTA ambaye
pia ni Makamu Mkuuwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Prof.Rwekaza Sympho
Mukandala amegomai kubadili matokeo ya Kidato cha Nne- 2012.
Chanzo
cha karibu cha Prof.Mukandala kinadai kuwa mara baada ya kutolewa
taarifa ya Serikali inayotaka 'kuboreshwa' kwa matokeo
hayo,Prof.Mukandala ameonesha kukataa amri hiyo hadi sasa.
"Sisi
tulipitisha matokeo hayo mbele yao na kwa idhini yao.Iweje leo Baraza
libadili matokeo?.Tunafanya hivi kwa faida ya nani na kwa ustawi wa
elimu ya wapi?" alinukuliwa akihoji Prof.Mukandala.
Habari
za kuaminka zinadai kuwa Prof.Mukandala pamoja na Katibu Mtendaji
Dr.Joyce Ndalichako wanajiandaa kuachia ngazi kama Serikali itasimamia
uamuzi wake huo.
Hata
hivyo, siku za hivi karibuni mwanahabari wetu alizungumza na
Ofisa Habari wa NECTA, John Nchimbi ambaye alisema wamekwishapokea
maelekezo kwa barua na kufanyia kazi ili kujitahidi ndani ya muda mfupi
matokeo yawe yametoka.
Nchibi
alikiri kuwapo kwa kasoro katika matumizi ya mfumo huo mpya wa
usahihishaji, kwani hawakushirikisha wadau wengi kabla ya kuanza
kutumia, lakini lengo la Baraza lilikuwa jema katika kukuza elimu nchini
“Kutokana
na tangazo hili, wanafunzi hawa wote hawana matokeo tangu juzi (
yalipofutwa bungeni ), hivyo wasubiri matokeo mapya yatakayotangazwa, na
waelewe wazi kuwa si lazima waliofeli wafaulu wote,” alisema Nchimbi.
No comments:
Post a Comment