Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, May 28, 2013

HUYU ndo Mganda aliye sajiliwa na SIMBA ambaye ni kiboko ya Ngassa

 
YANGA wamemsainisha Mrisho Ngassa wakachoonga, lakini Simba ilichofanya imetua Uganda, ikasajili bonge la beki wa kati ambaye kazi yake itakuwa moja tu kutuliza ukuta wa Msimbazi na kuzima nyodo za Ngassa.
Beki huyo Samuel Ssenkoomi anaichezea URA ya Kampala na Uganda Cranes ambapo mhariri wa michezo wa Gazeti maarufu la Newvision la Uganda, Fred Kaweesi aliiambia Mwanaspoti jana Jumatatu kwamba: "Simba imepata bonge la beki, Samuel anajua sana halafu hana papara."
Habari za uhakika ambazo Mwanaspoti ilizipata jana Jumatatu na kuthibitishwa na Kaimu Makamu Mwenyekiti wa Simba, Joseph Itang'are 'Mzee Kinesi' ni kwamba Simba imemsainisha beki huyo kwa mkataba wa miaka miwili.
Mzee Kinesi alisema mchezaji huyo amemalizana na Simba na atatua jijini Dar es Salaam wakati wowote tayari kujiunga na kikosi kitakachoanza mazoezi kesho Jumatano kwenye Uwanja wa Kinesi, jijini Dar es Salaam chini ya kocha mpya, Abdallah Kibadeni.
Simba ina imani kwamba kwa rekodi yake beki huyo ataweza kuzuia papara za mastraika wa Yanga, Ngassa, Didier Kavumbagu na wengine ambao Yanga inaringa nao.
Kinesi alisema: "Kocha Patrick Liewig tumeshamalizana naye na hatutaki hata kumsikia, alikuwa ana mambo fulani ya kubagua watu kitu ambacho si kizuri kwa kiongozi. Kibadeni tumemchukua kwavile ametupa ubingwa mara tatu anaijua Simba na atatujengea timu nzuri."
"Alishafanya hivyo kwenye timu ya vijana na mpaka sasa inafanya vizuri,"alisisitiza kiongozi huyo na kusema timu itaanza mazoezi kesho Jumatano kujiandaa na michuano ya Kombe la Kagame mwezi ujao nchini Sudan. Simba imepangwa kuanza na El Merreikh Juni 21.
Simba tayari imeshawasajili beki Issa Rashid wa Mtibwa, kipa Andrew Ntala wa Kagera, viungo Zahoro Pazi wa JKT Ruvu na Twaha Ibrahim wa Coastal. Wengine walioongezewa mkataba ni Haruna Chanongo, Ramadhani Singano na Abdallah Seseme.
Simba imepanga kuachana na kiungo wa Uganda, Mussa Mude kutokana na kutoridhishwa na kiwango chake. Hiyo ina maanisha kwamba kwa sasa Simba itakuwa na wachezaji wawili tu wa kigeni ambao ni Samuel na Abel Dhaira wote wa Uganda.
Felix Sunzu wa Zambia pamoja na Komanbilli Keita wa Mali wametemwa kama atakavyofanyiwa Mude.
source-mwanaspot
i

No comments:

Post a Comment