Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, May 26, 2013

JESHI LA POLISI LIMEENDELEA KUWATIA MBARONI WACHOCHEZI WA VURUGU ZA MTWARA


vujo-mtwara
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
Anuani ya Simu “MKUUPOLISI” & nbsp; Ofisi ya Inspekta Jenerali wa Polisi,
Simu : (022) 2110734 Makao Makuu ya Polisi,
Fax Na. (022) 2135556 S.L.P. 9141,
Unapojibu tafadhali taja: DAR ES SALAAM.
26 MAY 2013
TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI
Kwa mafanikio makubwa, Jeshi la Polisi nchini limeendelea kuwakamata wachochezi wanaotumia simu za mkononi (sms) ili kuchochea vurugu na fujo hapa nchini ambapo huko mkoani Lindi amekamatwa mtu mwingine mmoja kwa kufanya uhalifu huo.
Aidha, katika hatua nyingine, mtu aliyekamatwa jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kutuma meseji za uchochezi na kuhamasisha vurugu, Jeshi la Polisi limekamilisha upelelezi na ukusanyaji wa ushahidi na kesho atafikishwa makahamani.
Jeshi la Polisi linaendelea kukamilisha ukusanyaji wa ushahidi wa watu wanaofadhili, wanaosaidia na wanaoshawishi vitendo hivyo kutekelezwa ili na wao wafikishwe mahakamani mapema.
Katika kuhakikisha kwamba vitendo hivyo vinakomeshwa na kudhibitiwa hapa nchini, Jeshi la Polisi limeunda kikosi maalum toka makao makuu kwenda kusaidiana na makamanda wa mikoa ili kwa kusaidiana na wananchi kuweza kuharakisha ukamataji na watu wote wanaojihusisha na uchochezi wa vurugu na fujo kwa njia ya sms na kwa njia nyingine yeyote ile popote walipo ili waweze kufikishwa mahakamani haraka.
Jeshi la Polisi linawashukuru wananchi kwa ushirikiano wao mkubwa wa kutoa taarifa zinazofanikisha oparesheni hii, tunaomba waendelee kutuunga mkono kwa kutupatia taarifa zaidi na hata za watu wanaofadhili kwa njia ya pesa ama ushauri.
Jeshi la Polisi linatoa onyo kali kwa mtu yeyote ama kikundi cha watu wanaojihusisha na vitendo hivyo vya uchochezi kuacha mara moja. Aidha, litamkamata mtu yeyote anayejihusisha na vitendo hivyo vya uchochezi bila woga ama upendeleo pasipo kujali cheo, wadhifa, rangi ama umaarufu wa mtu huyo.
Imetolewa na:-
Advera Senso-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi (TZ)


TAARIFA YA JANA YA KIPOLISI NI HII HAPA ....



No comments:

Post a Comment