Franck Ribery ameapa kutoongea tena na mchezaji mwenzie wa Bayern Munich Jerome Boateng baada ya kulowanishwa kwa pombe wakati wa wakishangilia ubingwa wa Bundesliga wikiendi iliyopita.
Mfaransa huyo ambaye ni muislamu wa swala tano - alijaribu kukimbia ili aepuke ushangiliaji wa kumwagiana pombe wa wachezaji wenzie baada ya filimbi ya mwisho ya mchezo walioshinda 3-0 dhidi ya Augsburg.
Lakini pamoja na kujaribu sana kukwepa kuguswa na pombe - ambayo ni haramu kwa dini yake - Ribery hatimaye aliogeshwa na na Boateng.
Akiwa amekasirishwa kabisa kwa kitendo hicho cha mjerumani, winga huyo alisema: ‘Sitoongea tena na Boateng, anajua mie muislam. Nimeudhiwa sana na kitendo chake.’
Mlinzi David Alaba na kiungo Anatoliy Tymoshchuk pia walijiunga na Boateng kumlowesha Ribery, ambaye alionekana kutulia kwa wakati huo.
Golikipa Manuel Neuer kwa busara kabisa yeye alijiepusha na suala hilo na kuamua kuwamwagia baadhi ya mashabiki walionekana kupendezewa na ushangiliaji huyo.
PSPTB YATANGAZA MATOKEO YA MITIHANI YA MEI 2026: ASILIMIA 43.7 WAFAULU,
DIRISHA LA MITIHANI YA KATI KUFUNGULIWA JULAI 1, 2026
-
Na Janeth Raphael MichuziTv
Bodi ya Kitaaluma ya Ununuzi na Ugavi (PSPTB) imetangaza matokeo ya
mitihani ya 33 ya taaluma ya Mnyororo wa Ugavi iliyofanyik...
3 hours ago

No comments:
Post a Comment