


DDODMA.
KAMBI ya Upinzani Bungeni imetoa tuhuma nzito kwa Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahman Kinana ikidai kuwa anajihusisha na mtandao wa ujangili
nchini.
Hata hivyo, Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi amejibu tuhuma
hiyo akisema ni za uongo huku akiituhumu kambi hiyo kuwa imedanganya
wakati inajua ukweli kuhusu tuhuma dhidi ya Kinana.
Akiwasilisha maoni ya upinzani kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya
Wizara ya Maliasili na Utalii mwaka 2013/14, Msemaji wa Kambi ya
Upinzani kuhusu Maliasili, Mchungaji Peter Msigwa alisema vitendo vya
ujangili vimekuwa vikilitia doa taifa kwenye jumuiya za kimataifa.
No comments:
Post a Comment