Baada
ya Bunge kuahirishwa jana, nje ya ukumbi hali haikuwa nzuri baina ya
Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na Mbunge wa Same Mashariki
(CCM), Anne Kilango Malecela.
Mtafaruku
huo uliibuka baada ya Kilango kusikika akimtuhumu Lissu kwa uchochezi,
akisema kwamba amekuwa mbunge pekee anayeongoza kwa vurugu.
Maneno
hayo hayakumfurahisha Lissu ambaye alishindwa kuvumilia na kumgeukia
Kilango kwa nguvu huku baadhi ya wabunge wakishuhudia na wengine
wakimzuia Lissu.
No comments:
Post a Comment