Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, May 15, 2013

WATAALAM WA KUKABILIANA NA MAJANGA WAKUTANA


Picha na 1 
Viongozi wa serikali ya Tanzania na Marekani, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Shamsi Vuai Nahodha (kushoto) na Balozi wa Marekani nchini Tanzania Alfonso Lenhardt (kulia) wakionyesha nyaraka mbili za Mpango wa kukabiliana na maradhi ya mafua ya ndege. Nyaraka hizo zinahusisha vikosi vya jeshi na raia nchini Tanzania na Kamandi ya Jeshi la Marekani la Kupambana na Majanga Barani Afrika (USAFRICOM).Picha na Aron Msigwa – MAELEZO. Picha na 2 
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Shamsi Vuai Nahodha akizungumza na viongozi mbalimbali wa vitengo vya kukabiliana na majanga kutoka Tanzania na Marekani leo jijini Dar es salaam.Pamoja na mambo mengine amesema Tanzania inaendelea kujenga uwezo wa ndani wa kukabiliana na majanga mbalimbali.Picha na 3 
Balozi wa Marekani nchini Tanzania Alfonso Lenhardt akiongea na viongozi mbalimbali wa vitengo vya kukabiliana na majanga kutoka Tanzania na Marekani leo jijini Dar es salaam na kusisitiza kuwa serikali ya Marekani itaendelea kushirikiana na Tanzania na nchi nyingine katika kukabiliana na majanga yanayotokea. 
Picha na 7Washiriki wa mkutano wa siku 2 unaojadili namna ya kukabiliana na majanga mbalimbali na athari za Virusi vya mafua ya ndege wakiwa katika picha ya pamoja leo jijini Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment