Kijana William ambaye anadaiwa kufanya kazi ya utapeli katika majengo ya ibada
Kijana
William ambaye anadaiwa kufanya kazi ya utapeli katika majengo ya
ibada anapokuwa misikitini hutumia jina la Hassan Idd Lumbanga ambalo ni
la bandia.
Siku
zote za mwizi ni arobaini basi zilitimia kwa kijana huyo baada ya siku
hiyo kufika katika Msikiti wa Ijumaa Miyomboni akaungana na waumini
katika swala iliyokuwa ikiongozwa na Naibu Imamu wa Msikiti, Issa Boki,
ghafla (kijana huyo) alijiangusha chini na kujifanya amepoteza
fahamu .
Naibu
Imamu Boki aliliambia gazeti hili kuwa iliwalazimu kusitisha shughuli
za ibada na kutafuta gari harakaharaka na wakamkimbiza kijana huyo
katika hospitali ya mkoa ili akapatiwe tiba.
“Tulimuacha hapo hospitali
kwani alilazwa lakini baada ya sisi kuondoka alianza kufanya fujo
akahamishiwa wodi ya wenye mtindio wa ubongo, ambako nako alifanya
vurugu,” alisema Boki.
Akifafanua zaidi, kiongozi
huyo alisema walishitukia kijana huyo akiwa amerudi msikitini na kuanza
kuomba msaada wa nauli akidai anataka kurudi kwao Katavi.
“Alichangiwa shilingi hamsini
na tano elfu na mia mbili (55,200) wakati tunajiandaa kumpatia mmoja wa
waumini wetu alimtambua kuwa alimuona jijini Dar es Salaam katika
msikiti mmoja na akafanya kama alivyotufanyia sisi,” alisema Boki.
Naye Katibu wa Msitiki, Juma
Kibasila alisema baada ya madai hayo, walimhoji kijana huyo na akakiri
kuwa yeye ni tapeli na kwamba amekuwa akiishi kwa njia hiyo na
walipompekua walimkuta akiwa na funguo nyingi, hivyo kumkabidhi kwa
polisi wa kituo cha kati ambako aliwekwa korokoroni akisubiri upelelezi.
GPL.
No comments:
Post a Comment