Huyu ndiye Frank Ngowi muendesha baiskeli aliyegongwa na daladala, akionyesha jinsi alivyoumia baada ya kugongwa na daladala.
Baiskeli ya Frank Ngowi ikiwa kwenye eneo la ajali.
Hii ndio daladala iliyosababisha ajali na kukimbia lakini ilikamatwa na kurudishwa mpaka katika eneo la ajali..
Mashuhuda wa ajali hiyo wakiwa katika eneo la ajali.
Hawa
ndio vijana waliomkimbiza dereva wa daladala hadi kumkamata na hapo
ndio wapo kwenye harakati za kumrudisha kwenye eneo la ajali.
Gari ya polisi ikiwa imesha wasili katika eneo la ajali, likiwa na askari wa usalama barabarani tayari kupima ajali.
KATIKA
hali ya kusikitisha jamaa mmoja mkazi wa majengo mjini Moshi
anayefahamika kwa jina la Frank Ngowi amegongwa na Hiace (daladala)
yenye nambari za usajili T352 AFM inayofanya
safari zake za kutoka Kiboriloni mpaka mjini Moshi. Ajali hiyo
iliyotokea maeneo ya majengo polisi karibu na Kishamba Dispensary
imesababishwa na dereva aliyekua akiendesha daladala hiyo kulewa kupita
kiasi. Dereva huyo wa daladala ambaye jina lake halikuweza kufahamika
kwa haraka alipogundua amesha sababisha ajali alikimbia na kuelekea
maeneo ya majengo secondary ambapo waendesha bodaboda walimkimbiza na
kufanikiwa kumkamata na kumrudisha mpaka kwenye eneo la ajali.
No comments:
Post a Comment