Kileo alisema Langa alizidiwa ghafla juzi, wakamkibiza katika Hospitali ya Kairuki.
“Pale walituambia kwamba anasumbuliwa maralia kali pamoja na ugonjwa wa uti wa mgongo.
“Hivyo
tukalazimika kumkimbiza Muhimbili ambako alifikishwa katika chumba cha
watu matuhuti (ICU), leo ndiyo mauti yamemkuta,” alisema.
Kuhusiana na mazishi, Kileo alisema wanalazimika kumsubiri mkewe, Venus ambaye anatarajia kutua nchini kesho au keshokutwa.
“Mama yake yuko Marekani, hivyo tutamsubiri lakini tumeshazungumza naye.
“Sisi tutakaa leo kujadili suala hilo na wanafamilia na baadaye tutajua kila kitu,” alisema Kileo akionyesha utulivu.
Langa alikuwa akitamba na nyimbo yake mpya ya Rafiki wa Kweli iliyotengenezwa katika studio za Bongo Record chini ya P Funk.
Msanii
huyo alianza kutamba baada ya kushinda usakaji vipaji chini ya Coca Cola
na kuunda kundi la Wakilisha akiwa na Shaa au Sarah na Witness wakianza
na wimbo wao wa kwanza ‘Hoi’.
na global publisher
No comments:
Post a Comment