Huyu
mama alikaa juu ya paa kwa siku tatu tangu jumamosi kupinga nyumba yao
kuchukuliwa na bank.Anasema mumewe alimdhamini mtu alipochukua mkopo
bank miaka mingi iliyopita na kushindwa kulipa mkopo huo.(Picha ni kwa
Hisani ya Clouds Fm)
Huu ndio mwonekano mzuri wa mama wakati yuko juu ya paa la nyumba ambayo imechukuliwa na Benki ya Tanzania Investment bank(TIB)
Gea alimfata huko huko juu kumsikiliza na tumemsikia leo kwenye heka heka.Kesho pia itaendelea.
Nyumba
ipo mbezi Tangi bovu na inaeneo kubwa sana mama anasema hata akiuza si
chini ya millioni 500 na iweje atolewe kwa milioni 240? Wakati mdaiwa
nyumba zake mbili zimeshachukuliwa na mabasi mawili yale makubwa ya
safari za mikoani.Hiyo milioni 240 haijatimia tu? na kama bado kiasi
gani kimebaki?
Kwa mujibu wa maelezo yake kesi yao bado ipo mahakamani kwani tayari yule mdaiwa kuna mali zake zilizotaifishwa.
Mdaiwa
alikopa milioni 240 wameuza nyumba zake mbili (2) na mabasi mawili.
Wenyewe wanachodai katika hilo deni imebaki shilingi ngapi za kitanzania
na wao watoe maana wanauwezo wa kulilipa deni lililobaki ilinyuba yao
isichukuliwe na benki? Na kama nyumba ikiuzwa watoe deni la bank na hela
inayobaki wabaki nayo wao.
Maana
wakati haya yakiendelea hiyo jana inasemekana hii nyumba
imeshauzwa.Inauzwaje na shauri lipo mahakamani?Na jana mume wa huyu mama
alikuwa mahakamani maana ilikuwa siku ya kesi kuendelea kusikilizwa.
Na mumewe alirudi na oda maalum kutoka mahakamani kuwa nyumba hiyo isiguswe na vitu vyao virudishwe.
Inavyoonekana
hapa watu wameishakula pesa ili nyumba hii iuzwe wakati ni kinyume cha
sheria na istoshe kesi iko mahakamani kwa viongozi wetu jaribuni
kulifuatilia suala hili ili mwenye kupata haki yake apate na sio kutumia
mabavu wakati nchi hii ni yetu wote
PICHA NA HABARI KWA MSAADA WA GEA HABIB
No comments:
Post a Comment