MAHAKAMA ya Wilaya ya Iramba mkoani
Singida umemhukumu mwanamke mmoja mkazi wa kijiji cha Kisana wilayani humo,
Sayuni Ramadhani (42) kwenda jela miaka mitatu baada ya kukiri kosa la
kumng’ata mumewe sehemu zake za siri.Mwendesha mashitaka mkaguzi wa polisi,
Vincent Ndasa alidai mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Iramba,
Kariho Mrisho kuwa Juni 4 mwaka huu saa 12.00 jioni katika kijiji cha
Kisana, mshitakiwa kwa makusudi alizing’ata kwa meno sehemu za siri za
mume wake, Onesmo Nathania (42) na kumsababishia maumivu.Ndasa alidai kuwa siku
ya tukio, wanandoa hao waliporejea nyumbani kutoka kwenye klabu cha pombe
ya kienyeji kijijini hao, kulitokea kutokuelewana na hivyo kuanza
kugombana.Alidai wakati wanaendelea kupigana, Onesmo alizidiwa nguvu na
kuangushwa chini na mkewe ambaye alifungua zipu ya suruali na kufanikiwa
kuzitoa sehemu za siri za mumewe na kuzing'ata nusura azitenganishe.Mwendesha
mashitaka aliendelea kudai kuwa mlalamikaji Onesmo alipiga yowe na majirani
walifika mara moja na kumkimbiza katika zahanati ya kijiji kwa ajili ya
matibabu.Mshitakiwa alipoulizwa iwapo ni kweli alikiri kosa na
akaiomba mahakama imwonee huruma kwa kumpa adhabu ndogo kwa kuwa hilo lilikuwa
ni kosa lake la kwanza na kwamba anahitaji kuwa na mumewe ili waendelee kulea
idadi kubwa ya watoto wao kwa pamoja.Naye mwendesha mashitaka, Ndasa aliiomba
mahakama kumpa adhabu kali mshitakiwa ili kuwa fundisho kwake na pia kuogofya
wanawake wanaotarajia kuwafanyia unyama wa aina hii ya kung’ata sehemu nyeti za
waume zao.Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mfawidhi Mrisho, alisema mahakama yake
imezingatia kwa makini maombolezo ya mshitakiwa na kufikia uamuzi wa kutoa
adhabu ya kutumikia jela miaka mitatu.
Afya : Wadau washauri Bajeti mtazamo wa kijinsia kusaidia watoto Njiti
-
Na Deogratius Temba, Dar es salaam
Mtandao wa Haki ya afya ya uzazi umeshauri Serikali kutenga bajeti yenye
mtazamo wa Kijinsia katika sekta ya afya ili...
2 hours ago
No comments:
Post a Comment