skip to main |
skip to sidebar
MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KISUTU YAMWACHIA HURU, IDDY SIMBA JIJINI DAR ES SALAAM.
Idd Simba
HATIMAYE Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, hivi punde
imemwachiria huru Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Usafiri Dar es
Salaam (UDA), Idd Simba, Mkurugenzi wa Bodi hiyo ambaye alikuwa Diwani
wa Kata Sinza (CCM), Salum Mwaking’inda, Meneja Mkuu wa shirika hilo
Victor Milanzi
na Mkurugenzi wa Kampuni ya Simon Group , Simon Kisena waliokuwa
wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi wa shirika hilo kwa sababu
Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Dk.Eliezer Feleshi kuwasilisha hati ya
kutokuwa na haja ya kuendelea kuwashitaki washitakiwa hao chini ya
kifungu cha 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka
2002.
Simba anayetetewa na wakili maarufu nchini Alex Mgongolwa walifikishwa
na mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Mei 27 mwaka jana wakikabiliwa
na makosa ya kula njama,matumizi mabaya ya madaraka na kughushi na
hujumu uchumi.
Hivyo kuanzia sasa washitakiwa hao wapo huru
No comments:
Post a Comment