Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, June 6, 2013

MKUTANO WA SIKU MBILI WA TAASISI YA (BENJAMIN WILLIAM MKAPA HIV/ AIDS) WAFUNGULIWA JIJINI DAR ES SALAAM


SONY DSCWaziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Mheshimiwa Mizengo Kayanza Pinda akifungua wa mkutano wa siku mbili ulio wakutanisha wadau wa Taasisi ya Benjamin William Mkapa HIV/ AIDS, leo kwenye ukumbi Wa Nssf Waterfront Jijini Dar es Salaam.(PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE)SONY DSCWaziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Hawa Gahasia akielezea changamoto wakati wa mkutano wa siku mbili ulio wakutanisha wadau wa Taasisi ya Benjamin William Mkapa HIV/ AIDS, leo kwenye ukumbi Wa Nssf Waterfront Jijini Dar es Salaam.SONY DSCMkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Benjamin William Mkapa HIV/ AIDS,  Dr Ellen M konya Senkoro akielezea mafanikio ya Taasisi hiyoSONY DSCWadau mbalimbali wa Taasisi ya Benjamin William Mkapa HIV/ AIDS wakiwa kwenye mkutano huoSONY DSCWaziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Mheshimiwa Mizengo Kayanza Pinda,akiwa kwenye picha yapamoja  na wajumbe wa Bodi ya wadhamini ya (BMAF)mara baada ya ufunguzi wa mkutano huo

……………………………………………………….
                            Na Philemon Solomon                            
Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Mheshimiwa Mizengo Kayanza Pinda, amesema juhudi za makusudi zinafanyika katika kuimarisha sekta ya afya ili kujenga taifa lenye nguvu na lenye uwezo wa kuimarisha uchumi.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa siku mbili ulio wakutanisha wadau wa Taasisi ya Benjamin William Mkapa HIV/ AIDS, jana kwenye ukumbi Wa NSSF Waterfront Jijini Dar es Salaam Waziri Mkuu, amesema wanajamii wanapaswa kutambua michango mbalimbali ya kiafya inayotolewa na Taasisi kama hizo kwa kuwa zina manufaa makubwa kwa jamii nzima.
Pia, ameongeza kwamba hali inayopelekea kufanyika kwa juhudi hizo ni kuwepo kwa tafiti zinaonyesha kwamba wastani wa daktari mmoja mijini anahudumia wagonjwa 4,000 wakati Vijiji daktari mmoja anahudumia wagonjwa 100,000. Hali hii inasababisha mapungufu kwa upatikanaji wa huduma ya afya kwa muda mrefu katika hospitali na vituo mbalimbali vya afya.
Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Waziri Mhe. Hawa Ghasia amesema changamoto kubwa zinazo kabili sekta hiyo ni upungufu wa watumishi, miundombinu duni ya kazi na wafanyakazi kukaa zaidi mijini na kukwepa mazingira ya vijijini.
Pia ameongeza kwamba hali ya maambukizi ya ukimwi imepungua katika mazingira ya vijijini huku hali ikiwa tofauti na mjini kutokana na msongamano mkubwa wa watu uliopo katika maeneo ya mjini. Alisema pia kuwa takwimu zinaonyesha kuwa kina mama ndio wakionekana kuathirika zaidi na ugonjwa huo, hata kwa wale waliokuwa kwenye ndoa.
Waziri Ghasia aliendelea kusema kuwa huduma ya Taasisi ya Benjamini Mkapa HIV/AIDS  ilianza mwaka 2007 katika Halmashauri 33 tu na hadi sasa wamenenea Halmashauri 140 katika Wilaya 162 nchini. Hii ni asilimia 80 ya wilaya zote.
 Pamoja na changamoto zilizopo za kutafuta fedha na wadau kuwekeza kwenye sekta ya afya, kuna makampuni binafsi, msashirika na benki ambao wamechangia Taasisi hiyo kuweza kuboreshsa sekta ya afya, kwa kujenga nyumba za madaktari mikoani, kuboresha huduma ya ukimwi na pia afya yakina mama na watoto kwa kuhakikisha kuwa kuna wataalam katika wilaya hizo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo,  Dr Ellen Mkonya Senkoro, amesema “ Kwa kweli tumepata mafanikio makubwa sana kwenye kupunguza pengo la watumishi wa afya katika Halmashauri zaidi ya 135 nchini, na tangu tumepeleka wataalam, tumeona kuwa huduma  kwa wagonjwa zimeboreshwa na kutolowe kwa siku nyingi zaidi kwa wiki”
Mkutanio huu, unaokutanisha wadau wan je kama vile USAID, Global Fund,  Intrahealth, ITEC, WHO, Irish Aid, Abbot Fund na FHI pamoja na sekta binafsi, ambapo hii ni mara ya kwanza kushiriki kwao kwani wana mwaka tu tangu kufanya kazi na Taasisi hii. Wadau wa ndani ni kama vile Kibo Palace Hotel, Bank M, CRDB Bank, African Barrick Gold, NMB, Infotech Investment Group, MSD na wengine wengi.
Siku ya pili,6 Juni, 2013 Mhe. Rais Mstaafu, Benjamin William Mkapa ataongea kuhusu “ Private – Public Partnership in health sector” ikiwa ni mada kuhusu ushurikiano kati ya sekta binafsi na serikali kuwekeza kwenye sekta ya afya.

No comments:

Post a Comment