Balozi
wa Marekani Umoja wa Matifa Susan Rice ameteuliwa kuwa mshauri mpya wa
Usalama wa taifa wa rais Obama Jumatano, kitendo ambacho kimeleta
kasheshe kwa warepublikana ambao hawakufurahishwa hata kidogo hasa
ukizingatia ile kashfa ya Benghazi ambapo wamarekani waliuwawa na Balozi
Susan Rice kusema kuwa mashambulizi yale hayakupangwa ambapo baadaye
ilidhihirika kuwa sio kweli.
Rice
alionekana kuwa mtu ambaye angeweza kuchukua wadhifa wa Hilary Clinton,
kama waziri wa mambo ya nje , lakini baadae aliondoa jina lake kufuatia
ukosoaji wa warepublican. Wadhifa huo wa mshauri wa usalama wa taifa
hauhitaji idhini ya senate.
Bi
rice atachukuwa nafasi ya Tom Donilon, ambaye anatarajiwa kuondoka
mapema mwezi july. Bw. Donilon amekuwa mshauri mkuu wa sera za mambo ya
nje kwa rais Obama tangu kuchukuwa mamlaka hayo.
Bw.
Obama anasema Wamarekani wanapaswa kumshukuru sana Donilon kwa kusaidia
kumaliza vita vya Iraq, kumsaka na kuuawa gaidi wa Al Qaida, Osama bin
Laden, na kuborehsa uhusiano na washirika wetu.
No comments:
Post a Comment