Kamanda
mpya wa jeshi la polisi mkoa wa Singida ACP.Geofrey Kamwela akitoa
taarifa kwa waandishi wa habari (hawapo kwenye picha) juu ya kukamatwa
kwa Aziza Jumanne (19) mkazi wa kijiji cha Sughana jimbo la Singida
kaskazini kwa tuhuma ya jaribio la kuuwa mtoto wake wa kiume mwenye umri
wa siku kumi.(Picha na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu.
Jeshi
la polisi mkoani Singida linamshikilia mkulima Aziza Jumanne (19) mkazi
wa kijiji cha Sughana tarafa ya Mgori jimbo la Singida Kaskazini, kwa
tuhuma ya jaribio la kumtupa mtoto wake wa kiume mwenye umri wa siku 10
kwa lengo la kumuua.
Kamanda
wa Jeshi la Polisi mkoa wa Singida Geofrey Kamwela, amesema kuwa tukio
hilo la aibu na la kusikitisha, limetokea Juni 12 mwaka huu saa nane
mchana kweupe katika kijiji cha Sughana.
Amemtaja mtoto huyo mchanga wa kiume aliyetupwa na mama yake kuwa ni Akramu Alfa.
Kamwela
amesema siku ya tukio mama yake mkubwa na mtuhumiwa Mariamu Ramadhanai
alipata wasi wasi baada ya kutomwona Aziza akiwa muda mrefu bila kuwa na
mtoto wake mchanga.
Amesema “kutokana na wasi wasi huo, Mariamu aliweza kuita majirani kwa ajili ya kumhoji Aziza alikompeleka mtoto wake mchanga.
Baada
ya kumhoji Aziza aliweza kufunguka na hivyo kwenda kuonyesha mtoto wake
shambani alikomtupa na bahati nzuri, walikikuta kichanga hicho bado ki
hai”.
Kamanda
huyo amesema kuwa uchunguzi wa awali unaomyesha wazi kuwa Aziza
ametenda kosa hilo baya baada ya kutekelezwa na mwanaume aliyempa mimba
na kumzaa Akramu.
Hili ni tukio la pili ndani ya mwezi moja na nusu kwa watoto kutupwa na mama zao kwa lengo la kuwaua.
Mwishoni
mwa mwezi Mei mwaka huu, inadaiwa mwanafunzi wa Chuo cha Uhasibu tawi
la mkoa wa Singida, alimtupa mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miezi
mitano kwenye pagala la nyumba.
Kwa
mujibu wa Kamanda Kamwela hadi sasa mzazi huyo hajulikani alikokimbilia
na mama yake mzazi kutoka Babati alifika ili amchukue mtoto huyo
aliyetekelezwa, lakini hakuweza kukabidhiwa kwa madai hakuna ushahidi wa
kuonyesha amezaliwa na mtoto wake aliyekuwa akisoma uhasibu.
No comments:
Post a Comment