Ambrose
Hakimu wa
Mahakama ya Wilaya ya Arumeru, Devotha Kamuzora jana alimkabidhi hati
ya mashitaka yanayomkabili, Victor Ambrose (20) ambaye ni mtuhumiwa
pekee aliyepandishwa kizimbani baada ya kutokea shambulio la bomu
katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Olasiti jijini Arusha.
Ambrose alikabidhiwa hati hiyo ya mashitaka yanayomkabili jana katika
Mahakama ya Wilaya ya Arumeru jijini Arusha na kuambiwa na wakili wa
Serikali, Adelaide Kasala kuwa upelelezi dhidi ya kesi hiyo,
haujakamilika na kumuomba Hakimu Kamuzora kutaja tarehe nyingine.
Hakimu Kamuzora kabla ya kuahirisha kesi hiyo alimuuliza Ambrose kama
alipewa hati yake dhidi ya mshitaka yanayomkabili. Ambrose alipojibu,
“hapana.” Baada ya jibu hilo,
Hakimu alitoa
hati hiyo na Ambrose kukabidhiwa na kuahirisha kesi hiyo hadi Juni
24.Ambrose ambaye ni dereva wa bodaboda na mkazi wa Mrombo jijini
Arusha, mara ya kwanza alifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi jijini
Arusha na baadaye kuhamishiwa Mahakama ya Wilaya ya Arumeru na kusomewa
mashitaka yake kwa mara ya tatu sasa huku akitakiwa kutojibu lolote,
kutokana na Mahakama hiyo kutokuwa na uwezo kisheria wa kusikiliza kesi
za mauaji.
Wakili wa Serikali, Adelaide Kasala alidai mahakamani hapo Victor
alitenda makosa hayo Mei 5, mwaka huu katika Kanisa la Mtakatifu Joseph
Mfanyakazi, Olasiti jijini.
No comments:
Post a Comment