Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe ACP Fulgency Ngonyani akizungumza na
mwandishi wa Mtandao Huu bwana Prosper Mfugale Juu ya Tukio Hilo.
.
Mkazi
Mmoja wa Mtaa wa Idundilanga Mjini Njombe Yasinta Mdetele Mwenye Umri
wa Miaka 25 Amefariki Dunia Wakati Akijaribu Kutoa Mimba.
Kamanda wa Polisi Mkoani Njombe Fulgency
Ngonyani Amethibitisha Kutokea Kwa Tukio Hilo na Kusema Kuwa Tukio Hilo
Limetokea June Tano Mwaka Huu Majira ya Saa Tatu Asubuhi Baada ya Kunywa
Kinywaji Kinachodaiwa Kuwa na Sumu.
Amesema Marehemu Alikutwa Chumbani
Kwake Akiwa Amefariki Huku Pembeni Yake Kukiwa na Mtoto wa Kike Ambae
Pia Alikutwa Amefariki na Kuongeza Kuwa Marehemu Hakuacha Ujumbe Wowote
na Hakuna Mtu Yoyote Anaeshikiliwa Kutokana na Tukio Hilo.
Ameongeza Kuwa Jeshi la Polisi
Linaendelea na Uchunguzi wa Tukio Hilo na Kutoa Wito Kwa Wananchi Kuacha
Vitendo Vya Utoaji Kwani ni Kosa la Kisheria na Pia Linaweza
Kuhatarisha.
No comments:
Post a Comment