Hii post ya Salma ni ya June 4 2013
Baada ya watu wengi kuzipata habari na bila kujua imekuaje
kwa Mtanzania anaedaiwa kukamatwa na dawa za kulevya nchini Egypt na
kwamba alikua anakaribia kunyongwa, balozi Mohamed Haji wa Tanzania
nchini Egypt ameongea Exclusive na millardayo.com na kueleza yote
anayoyafahamu kuhusu hii ishu.
Namkariri akizungumza
1. Ni kweli kuna raia wawili Watanzania wamekamatwa na dawa
za kulevya ambao ni Mbarak Abdallah Salim (28) na Sharifa Mahmud (27)
wakazi wa Magomeni Kagera Dar es salaam, wanaundugu wa mtoto wa shangazi
na mjomba.
2. Walikamatwa tarehe 16 May 2013 wakati wakiingia Misri, kwa
mujibu wa maelezo safari yao ilianzia Dar es salaam kwenda Mombasa,
Nairobi mpaka Misri.
.
3. Dawa za kulevya walizokamatwa nazo zimetajwa kwamba ni Heroine kilo saba.
4. May 18 2013 ndio tuliitwa kwenda kutazama Raia wetu,
nikatuma maafisa wawili wazuri kwenda kutazama ili raia wetu
wasimbambikiwe kesi.
5. Baada ya hapo waliwekwa rumande na tukapata nafasi ya
kuwaunganisha na nyumbani huku Tanzania wakaongea kwenye simu
kilichowapata.
6. 26 May 2013 ndio walipelekwa Mahakamani kwa mara ya kwanza na kurudishwa rumande wote wawili.
7. Hawa ndio Watanzania wa kwanza kukamatwa na kesi kama hii
na ikithibitishwa wamefanya kweli, hili kosa ndilo litakua doa la kwanza
kwa Tanzania hapa Misri.
8. Ishu ya kunyongwa, tunajaribu kufanyia kazi lakini hakuna
kumbukumbu za mgeni yeyote kwa sisi tunavyojua ambae amewahi kunyongwa
kuhusu ishu ya dawa za kulevya.
9. Tunajitahidi kuwasiliana na mamlaka zinazohusika ili kujua
siku gani watapelekwa tena Mahakamani alafu tutawafahamisha nyumbani.
CHANZO MILLARD AYO
No comments:
Post a Comment