Kwa mara nyingine Bendera ya Tanzania imeendelea kupepea katika Tasnia ya Ulinzi wa Amani ya Kimataifa.
Mapema
wiki hii, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon na Mwenyekiti
wa Umoja wa Afrika Bi. Nkosizana Dlamin Zuma wametangaza uteuzi wa
Luteni General Paul Ignace Mella Kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (
JWTZ) kuwa Mkuu Mpya wa Jeshi la Kulinda Amani la Umoja wa Mataifa
huko Darfur ( UNAMID)
Taarifa
iliyotolewa na Ofisi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon,
na nakala yake kutumwa katika Uwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, imeeleza kwamba, Lt. Gen.
Mella anachukua nafasi iliyoachwa na Mkuu wa zamani wa Jeshi hilo
(UNAMID), Lt. Gen Patrick Nyamvumba kutoka Rwanda ambaye amemaliza muda
wake wa utumishi March 31,2013.
Wasifu
wa Luteni General Paul Ignace Mella unaelezwa kuwa ni Mwanajeshi wa
muda mrefu na mwenye uzoefu na utumishi uliotukuka katika JWTZ akiwa
amewahi kushika nyadhifa mbali mbali muhimu za uongozi.
Baadhi
ya nyadhifa hizo ni pamoja na Naibu Kamanda Kikosi cha Tanzania chini
ya Umoja wa Mataifa huko Liberia ( 1993-95), Kamanda wa Kikosi
cha JWTZ, Afisa Mnadhimu-Makao Makuu ya Jeshi, Mwambata Jeshi-Ubalozi
wa Tanzania Uganda na hadi sasa alikuwa ni Mkuu wa Usalama na Utambuzi-
JWTZ.
Uteuzi
wa Lt. Generali Mella unafuatia mchakato mrefu ulioshindanisha
wateuliwa kutoka nchi mbalimbali duniani, na hatimaye yeyé akaibuka
mshindi.
OFISI YA UBALOZI WA TZ UN
No comments:
Post a Comment