MSAJILI
wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa amekipa usajili wa kudumu Chama
cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) huku akivitaka vyama vya siasa kufuata
sheria na kuepuka kuwa vyanzo vya vurugu na uchochezi wa migogoro.
Tendwa
ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akiwakabidhi cheti
cha usajili wa kudumu viongozi wa chama kimpya cha kinachojulikana kama
Chama cha Ukombozi wa Umma.
Tendwa Akipa Usajili wa Kudumu Chama Kipya cha 21, CHAUMMA
Na Thehabari.com
Alivitaka
vyama vya siasa kuhakikisha vinatimiza malengo yao ya kushika dola na
hata kama itashindikana kwao, basi kuhakikisha wanapata nafasi za
uwakilishi wa wananchi zikiwemo za udiwani, ubunge pamoja na uongozi wa
serikali za mitaa kwa mujibu wa taratibu za nafasi hizo.
Alisema
kwa sasa vipo vyama vya siasa ambavyo licha ya kuwa na usajili wa
kudumu na uongozi mzuri usio na migogoro vimeshindwa kutimiza malengo ya
msingi ya chama kwa kushika nafasi za uwakilishi maeneo anuai kwa
mujibu wa utaratibu.
"…Vyama
hivi unakuta hawana mbunge, hawana diwani, hawana viongozi serikali za
mitaa, kijiji na kwingineko lakini ukiangalia wana viongozi wazuri
hawana migogoro ndani ya chama, haya sio madhumuni ya chama cha siasa,"
alisema Tendwa.
Aidha
aliwataka viongozi wa CHAUMMA kuhakikisha wanajipanga vizuri ili waweze
kutimiza malengo ya chama na kuwawakilisha wananchi maeneo mbalimbali
ya uongozi kisiasa. Alisema katika mapendekezo mapya ofisi yake
inafikiria kuanza kuvipunguza vyama ambavyo licha ya kuwa na usajili
havifanyi chochote kama ilivyo kwa madhumuni ya kuanzisha chama.
"Sheria
inafanyiwa marekebisho, chama kikikaa ndani ya miaka mitano hakijafanya
chochote tunafikiria kukifuta, kiongozi wa chama akitukana miezi sita
unafungiwa kwa muda…maana hatuwezi kuruhusu matusi, vurungu na masuala
mengine yasiokuwa na msingi ndani ya vyama vya siasa," alisema Tendwa.
Hata
hivyo amesema katika mapendekezo yao ya mabadiliko ya katiba
wamependekeza mambo mengi ikiwemo sasa kuruhusu vyama kujiunga na
kufanya shughuli za siasa kama ilivyo kwa nchi za Kenya, Afrika Kusini,
Lethoto na nchini Namibia.
Akizungumza
mara baada ya kukabidhiwa cheti cha usajili wa kudumu Mwenyekiti wa
muda wa CHAUMMA, Wallance Mayunga alisema wamejipanga vizuri katika
kuwatumikia wananchi na chama chake kinatambua changamoto zilizopo
nchini katika uongozi, utendaji na utawala hivyo kina nia ya kuleta
mabadiliko.
Nafasi
ya Katibu Mkuu wa muda wa CHAUMMA inashikiliwa na Shaffii Abed huku
Hamad Tao akiwa ni miongoni mwa wanachama waanzilishi wa nchama hicho.
No comments:
Post a Comment