Mwakilishi
wa kampuni ya Steps Solar, Johnson Mwamba (mwenye koti) akizungumzia
udhamini wa kampuni yao katika tuzo za Steps Movie Award
zilizopangwakufanyika Jumamosi kwenye ukumbi wa Blue Pearl. Meneja
Masoko wa Steps Entertainment, Kambarage Ignnatus akionyesha moja ya
tuzo zitakaotolewa kwa wasanii sikuya Jumamosi kwenye ukumbi wa Blue
Pearl, Ubungo Plaza, kulia ni Mwakilishi wa kampuni ya Steps Solar,
Johnson Mwamba.
Na Mwandishi Wetu
Kampuni
ya usambazaji wa filamu Tanzania ya Steps Entertainment limited
Jumamosi itatoa tuzo kwa wasanii, Watayarishaji, Waongozaji, na wadau
mbalimbali waliopo katika tasnia ya filamu Tanzania.
Mratibu
wa tuzo hizo, Carlos Johns Silondwa alisema kuwa tuzo hizo zitafanyika
kwenye ukumbi wa Blue Pearl Ubungo Plaza na zitawahusisha zaidi wasanii
wanaofanya kazi na kampuni yao tu.
Silondwa
alisema kuwa kutakuwa na vipengele nane ikiwa pamoja na Filamu Bora ya
Mwaka, Kampuni iliyotengeneza filabu bora, msanii anayependwa na watu
ndani na nje ya mwisho, msanii bora chipukizi, muigizaji bora wa kike,
muigizaji bora wa kiume, muongozaji bora wa filamu na mwandishi bora wa
filamu.
Silondwa
alisema kuwa wameandaa tuzo hizo kwa lengo la kuanzisha tuzo hizo ni
kuleta ushindani na kukubali mchango wa wasanii, watayarishaji na wadau
wote kampuni inatumia fursa hii ya kuwatambua na kujali mchango wa
wasanii katika ukuzaji wa filamu nchini Tuzo ni kichocheo kitakacholeta
ushindani unaoweza kujenga tasnia ya filamu na kujenga ajira kwa jamii
kubwa.
Alisema
kuwa tuzo hizo zimezingatia michango mbalimbali kutoka kwa wadau
mbalimbali ambao wamekuwa mbele katika kutangaza tasnia ya filamu ndani
na nje ya nchi kupitia njia mbalimbali, pia kutakuwa na tuzo za heshima
kwa waliotangulia kuitambulisha tasnia ya filam u Tanzania.
“Tunaamini
kuwa tuzo zitakuwa kichocheo kikubwa cha kukuza tasnia ya filamu
kuongeza ushindani katika kutengeneza filamu Bora, hadithi nzuri
zinazoelimisha, kukuza na kuitangaza lugha ya Kiswahili nje ya mipaka ya
Tanzania lugha ambayo imekuwa ikukua kila siku kwa kupitia filamu za
kitanzania zinazopenyeza na kuvuka mipaka ya nchi,” alisema Silondwa.
Alisema
kuwa wanaarajia kuwa na Tuzo kubwa zitakazoshirikisha wadau wote kwa
baadae, na kuwa ni moja kati ya moja ya kampuni wadhamini wa tuzo zenye
mlengo wa kimataifa, mwaka huu kampuni imeandaa tuzo hizo pasipo
kuwatumia wadhamini wa nje ya kampuni ikipata udhamini kwa kampuni ya
Steps Solar pekee
No comments:
Post a Comment