Na Mwandishi WetuHOSTI wa Kipindi cha ‘The Mboni Show‘ kinachorushwa kupitia Kituo cha Runinga cha EATV, Mboni Masimba Jumapili iliyopita aliangua kilio mbele ya Rais Mstaafu wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi walipokuwa kwenye hafla ya kufuturisha kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Baada ya kutoa shukrani alionekana kuwa mwenye furaha kwa kumtambulisha baba yake mzazi, mzee Masimba ambaye hajulikani kwa watu kama ilivyo kwa mama yake.
“Nakuomba msamaha mama yangu, Mboni si yule tena nimebadilika, nisamehe sana,“ alisema Mboni kisha akaangua kilio kujutia makosa yake.
Baada
ya tukio hilo, Mboni alisikika akiomba dua kwa Mwenyezi Mungu ili ampe
mume mwema. Mtangazaji huyo alirudia mara kwa mara kipengele hicho cha
kuomba mume kiasi cha baadhi ya wageni waalikwa kusema kwamba ni kweli
anahitaji mume kwani umri wake unahitaji kuwa na familia.Wengine ni Shay-rose Bhanji na baadhi ya wanamuziki wa The Kilimanjaro ‘Wana Njenje’ Steve Nyerere na watu wengine maarufu.
Habari imeandikwa na Hamida Hassan, Imelda Mtema, Musa Mateja na Shakoor Jongo.

No comments:
Post a Comment