“PRESS RELEASE”
TAREHE 31. 07. 2013.
WILAYA YA MBEYA MJINI -
AJALI YA MOTO
MNAMO
TAREHE 30/07/2013 MAJIRA YA SAA 20:30HRS – HUKO SOKOMATOLA JIJI NA MKOA WA
MBEYA. ASHA D/O ABDALLA, MIAKA 90, MHEHE, MKULIMA NA MKAZI WA SOKOMATOLA
ALIUNGULIWA NYUMBA YAKE NA KUSABABISHA HASARA YA KUUNGUA KWA PAA LA NYUMBA
YAKE, MADIRISHA PAMOJA NA VITU VILIVYOKUWA NDANI AMBAVYO THAMANI YAKE BADO
HAIJAFAHAMIKA. CHANZO CHA MOTO HUO INADHANIWA KUWA NI HITILAFU ZA UMEME. HAKUNA
MADHARA YA KIBINADAMU YALIYORIPOTIWA KUTOKEA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUWA NA
TAHADHARI NA MAJANGA YA MOTO ILI
KUEPUKANA NA MADHARA YANAYOWEZA KUJITOKEZA.
WILAYA YA MBEYA -
KUPATIKANA NA MIRUNGI
MNAMO
TAREHE 30/07/2013 MAJIRA YA SAA 22:00HRS
HUKO ITEWE JIJI NA MKOA WA MBEYA, ASKARI
POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA NTOKAMBALI S/O SINGINALI, MIAKA 27, MSAFWA, NA
MKAZI WA ITEWE AKIWA NA MIRUNGI KG. MOJA NA NUSU [1.5] NDANI YA MFUKO MWEUSI
WA RAMBO. MTUHUMIWA NI MTUMIAJI WA MIRUNGI HIYO AMEKAMATWA NA TARATIBU
ZINAANDALIWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA
MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA
KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
WILAYA YA MBEYA –
KUPATIKANA NA BHANGI
MNAMO
TAREHE 30/07/2013 MAJIRA SAA 02:30HRS NSONGWI JUU JIJI NA MKOA WA MBEYA, ASKARI
POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA MAULID S/O CHARLES,MIAKA 25, MSAFWA, NA MKAZI
WA UYOLE AKIWA NA BHANGI ROBO KILO [¼]
NDANI YA MFUKO MWEUSI WA RAMBO .
MTUHUMIWA NI MTUMIAJI NA MUUZAJI WA BHANGI HIYO AMEKAMATWA NA TARATIBU
ZINAANDALIWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA
MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA
KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
Imesainiwa na,
[DIWANI ATHUMANI - ACP]
KAMANDA WA POLISI
MKOA WA MBEYA
No comments:
Post a Comment