Mkurugenzi
wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato
Tanzania(TRA) Bw. Richard Kayombo(kulia) akieleza kwa waandishi wa
habari kuhusu mfumo mpya wa ulipaji kodi za magari kwa njia ya mtandao,
kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo ukumbi wa Idara ya
Habari kushoto ni Meneja wa Mradi wa Mamlaka hiyo Bw. Ramadhani
Sengali.PICHA ZOTE NA HASSAN SILAYO
Kaimu Meneja Magari kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) Bw. Julius Mchihiyo (kulia)akitoa ufafanuzi juu ya utekelezaji wa mfumo mpya wa ulipaji kodi za magari kwa njia ya mtandao, kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo ukumbi wa Idara ya Habari kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Bi. Zamaradi Kawawa.
Kaimu Meneja Magari kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) Bw. Julius Mchihiyo (kulia)akitoa ufafanuzi juu ya utekelezaji wa mfumo mpya wa ulipaji kodi za magari kwa njia ya mtandao, kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo ukumbi wa Idara ya Habari kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Bi. Zamaradi Kawawa.
Kuanzia
mwezi Agosti 2013 malipo yote ya ada za mwaka za magari (annual road
license) yatafanywa kwa njia ya mtandao kwa maana ya kutumia simu za
kiganjani, benki na wakala wa Maxmalipo.
Hii inatokana na maboresho ya mifumo
ya kielektroniki ambayo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inaendelea
kuyafanya ikiwa ni juhudi za kutoa huduma bora kwa walipakodi na
kuhakikisha kuwa mapato ya Serikali yanayokusanywa na yanawasilishwa kwa
wakati kwenye mfuko mkuu wa Serikali, Benki Kuu.
Mfumo huu utatumika kulipa ada za mwaka za magari ambapo mlipakodi anaweza kupata taarifa ya kiasi cha kodi anachotakiwa kulipa.
Faida za mfumo.
Mfumo huu umeanzishwa kutokana na faida nyingi kama:Mfumo huu ni rahisi kutumia na utapunguza misongamano isiyo ya lazima katika ofisi za Mamlaka ya Mapato na benki na hivyo kumwezesha mlipakodi kulipa ada ya gari lake akiwa mahali popotenchini.Mfumo huu una panua wigo wa njia za kulipa kodi kwah
iyo unampa mlipakodi uhuru wa kuchagua njia ambayo anaona ni rahisi kutumia kutokana na mazingira atakayo kuwamo.Vilevile kwa kutumia utaratibu huu mlipakodi anaweza kuhakiki kiwango cha ada ya gari anachotakiwa
kulipa na hivyo kuepuka udanganyifu unaofanywa na vishoka ambao
huwarubuni wananchi kwa kuwapa taarifa za viwango vya ada za magari
visivyo sahihi.Mfumo huu ni salama kwani kuna uhakika kwamba malipo yote ya kodi yanakwenda Benki Kuu kwani unaondoa mwingiliano wa wafanyakazi wa TRA na walipakodi.Kwa upande mwingine mfumo huu unaiwezesha TRA kukusanya kodi kwa gharama nafuu.
Utaratibu wa kutumia mtandao kulipa ada za magari ni kama ifuatavyo:Kufahamu kiwango cha kodi. Tuma ujumbe wenye neno“Kadiria”au“Assess”acha nafasi andika namba za garimfano KADIRIAT171AUCkwenda namba 15341.Kulipa: Tuma ujumbe wenye neno;“sajili”acha nafasi na kuandikanamba ya gari husika. Tuma ujumbe huo kwenda namba 15341. Baada ya hapo mlipakodi atapataujumbe wa namba ya kumbukumbu ya malipo (Reference number).Fanya malipokwa kutumiaTIGOPESA,MPESA, AIRTELMONEY au wakala wa MAXMALIPO kwa kutumia namba ya kumbukumbu uliyopata.Kuchukua cheti: (sticker ya gari):nenda katika ofisi yoyote ya TRA ukiwa nanamba ya kumbukumbuuliyoitumia kufanya malipo.
Zingatia.
Ili kuweza kuchukua kadi ya gari mlipakodi anatakiwa kuwa
na kitambulisho chochote kama vile kitambulisho cha Taifa, Hati ya
kusafiria, Lesseni ya udereva, Kitambulisho cha mpiga kura n.k.
Mfumo wa kulipa ada
za magari za mwaka ni muendelezo wa maboresho ya mfumo wa kulipa kodi
kwa mtandao (Revenue Gateway) ambao ulibuniwa na TRA kwa kushirikiana na
Benki Kuu (BOT). Mfumo huu umeanza kutumika rasmi Julai Mosi 2013.
Mfumo wa RG
pamoja na kuwa unaunganisha mifumo ya TRA na Benki Kuu pia
unaiunganisha TRA na walipakodi, Benki za Biashara, Makampuni ya simu
(M-PESA, TIGOPESA, AIRTELMONEY n.k) pamoja na wadau wengine kama vile
Hazina na NIDA.
No comments:
Post a Comment