Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, July 3, 2013

MKUTANO WA WAKE WA MARAIS WA NCHI ZA AFRIKA WAMALIZIKA SERENA HOTEL JIJINI DAR ES SALAAM.

Copy of IMG_4367Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akihojiwa na Mtangazaji, Adesewa Josh kutoka  Channels TV ya nchini Nigeria wakati wa mkutano wa wake wa Marais wa nchi zaa Afrika unaofanyika katika hoteli ya Serena hapa Dar es Salaam tarehe 3.7.2013.
Copy of IMG_4407Copy of IMG_4408Baadhi ya washiriki wa mkutano wa wake wa marais wa Afrika wakisikiliza hotuba ya Rais Jakaya Kikwete alipohutubia mkutano huo tarehe 3.7.2013.Copy of IMG_4425Rais Jakaya Kikwete akihutubia mkutano wa siku mbili wa wake wa marais wa Afrika unaofanyika katika hoteli ya Serena hapa Dar es Salaam.
Copy of IMG_4515Rais Jakaya Kikwete akiwa na Rais Mstaafu wa Marekani Mheshimiwa George Bush na mke wake Mama Laura Bush pamoja na Mama Salma Kikwete wakiangalia igizo lililokuwa linafanya na kikundi cha Tanzania House of Talent wakati wa mkutano wa wake wa marais wa Afrika unaofanyika katika hoteli ya Serena tarehe 3.7.2013.IMG_4562Rais Jakaya Kikwete akiwa na mgeni wake Rais Mstaafu wa Marekani Mheshimiwa George Bush wakiwa katika picha ya pamoja na wake wa marais wa Afrika  na wana kikundi cha Tanzania House of Talents mara baada ya kufanya igizo kwenye mkutano wao kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam tarehe 3.7.2013.
PICHA  NA JOHN LUKUWI

No comments:

Post a Comment