Na Father Kidevu Blog
MAZISHI ya Mwanafunzi na Rais wa Taasisi ya wanafunzi AIESEC- IFM, Wende Lwendo wa Mwaka wa Kwanza Uhandisi Kompyuta wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) aliyefariki juzi kwa kufa maji baharini yanafanyika kesho.
Wende
, alifariki katika ufukwe wa bahari ya Hindi eneo la Kipepeo Kigamboni
jijini Dar es Salaam akiogelea na wenzake watatu majira ya jioni baada
ya kumaliza mitihani yao ya kufunga mwaka wa masomo.
Kaka
wa marehemu, Sammy Lwendo ameiambia Father Kidevu Blog leo kuwa
marehemu anataraji kuzikwa kesho alasiri katika makaburi ya Kinondoni na
mipango yote ya mazishi inaendelea vizuri.
Lwendo
amesema kuwa mipango ya mazishi ilikuwa ikisubiri wazazi wa marehu
ambao waliwasili juzi usiku wakitoakea mkoani Arusha na kutaarifu ndugu
kuwa mazishi yatafanyika Dar es Salaam.
"Marehemu
Wende, anataraji kuzikwa Makaburi ya Kinondoni kesho lakini kabla ya
mazishi kutakuwa na ibada itakayofanyika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri
Tanzania (KKKT) Usharika wa Kinondoni, "alisema Lwendo.
Lwendo
amesema ibada hiyo itaanza majira ya saa 8:00 mchana ambapo pia ndugu
jamaa na marafiki watapata wasaa wa kutoa heshima za mwisho kwa marehemu
Wende.
Mmmoja
wa wanafunzi wa IFM, Ester Boswell, ambaye walikuwa wakishi chumba
kimoja na marehremu huko Kigamboni ameelezea msiba huo kuwa ni pigo
chuoni kwao na kwake kwani Marehemu alikuwa ni rafiki yake mkubwa si
chuoni lakini hata kabla hawajajiunga na chuo hicho.
Boswell
amesema kuwa Marehemu alikuwa ni Rais wa taaasisi ya Wanafunzi wa IFM
ijulikanayo kama AIESEC na alikuwa mhim,ili mkubwa wa taasisi hiyo.
Aidha
amesema kuwa hadi sasa binafsi haamini kifo cha Wendi, huku akielezea
kuwa Marehemu alikuwa ni mtu mcheshi na kuogelea ilikuwa ni moja ya vitu
vikubwa anavyo vipenda.
"Marehemu
alikuwa mpenzi kumbwa sana wa kuogelea na siku zote alikuwa anapenda
kwqenda kuogelea na hata anapokuwa mpweke hosteli huamua kwenda Beach
kuogelea na siku ya tukio aliniaga kuwa anaenda kuogelea na wanafunzi
wengine wakiwapo wazungu ambao wapo katika kubadilishana uzoefu wa
kimasomo," alisema Boswell.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam ukisubiri maziko.
No comments:
Post a Comment